Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. Davidi Mwakyusa akizungumza na Naibu Waziri wa Afya Dkt Aisha Kigoda(katikati) na katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Blandina Nyoni (kulia) mara baada ya uzinduzi wa mabaraza ya Wataalam wa Huduma za Maabara za Afya na Wataalam wa Radiolojia leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO
Serikali imewataka wataalam wa maabara za afya na radiolojia nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni na maadili ya taaluma zao ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wanaowahudumia.
Kauli imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa wakati wa akizindua mabaraza ya wataalam wa radiolojia na huduma za maabara za afya nchini.
Amesema watumishi wa afya kazi yao ni kuboresha hali ya afya kwa wananchi kwani ndio waajiri wao huku akiwataka kutambua umuhimu wao katika taifa na jinsi walivyo na wajibu wa kutoa tiba sahihi kwa wananchi.
“Tunajua fika kwamba kufanya utambuzi sahihi (correct diagnosis) ndiyo mwanzo wa kumpatia mgonjwa tiba sahihi, tiba isiyo sahihi inaweza kuchelewesha kupona kwa mgonjwa au mgongonjwa anaweza kupata kilema au hata kupoteza maisha kabisa “amesisitiza.
Waziri Mwakyusa amekemea tabia ya baadhi ya wataalam ambao hudai pesa na kutumia lugha mbaya kwa wagonjwa na wakati mwingine wanajisahau na kufanya kazi kama madaktari jambo ambalo si sahihi kwa mujibu wa taaluma zao.
“Wapo wataalam wanaojisahau na kufanya kazi kama madaktari ,baadhi wanatibu wagonjwa au wanawaambia wagonjwa matatizo yao.Hii si kazi yao na wanapofanya hivyo wanaweza kuleta hofu isiyo ya lazima na mtafaruku kwa wagonjwa” amefafanua.
Ameongeza kuwa mazingira hayo ya kutokuzingatia kanuni na maadili kwa wataalam wa maabara za afya na radiolojia yanahitaji kuwekewa kanuni madhubuti ili kuwabana wachache wanaopaka matope taaluma hizo.
0 comments:
Post a Comment