MISS TOTOZ KUMEKUCHA, KUFANYIKA TEMEKE SIKU YA NANE NANE!!

Na Shaban Mpalule.
Shindano la kumsaka mlimbwende wa watoto wilaya ya Temeke, Miss Totoz litafanyika siku ya nane nane katika ukumbi wa ikweta Grill uliopo Temeke Mtoni kwa Azizi Ali kwa kushirikisha watoto warembo mbalimbali kutoka katika vitongoji vyote vya wilaya ya Temeke.
Akizungumzia shindano hilo mratibu kwa upande wa Temeke Jacqueline Magayane, aalisema kuwa mpaka sasa warembo wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa equator Grill kuanzia saa nane mchana hadi kumi na mbili jioni.
“kwa ujumla kila kitu kinakwenda vizuri, watoto wote ni bomba, na wamejitokezaa kwa wingi kushiriki shindano hili, ambalo litawafanya watoto kukua wakijua nafasi ya vipaji vyao na wanawea kuwa wawakilishi bora katika mashindano ya vodacom kwa miaka ijayo, na pia ni changamoto kwa watoto pia kuhusiana na shindano hili” alisema JackNa kuongeza kwamba washiriki wote watapita katika jukwaa zaidi ya mara nne wakiwa katika mavazi ya tofauti ikiwepo vazi la Ufukweni, vazi la Ubunifu, na vazi la kutokea sambamba na kuonyesha vipaji vyao kwa kila mshiriki.
Warembo wanaoendelea na mazoezi kila siku chini ya Mwalimu wao Miss Iringa 2009 Witness Tresphory ni pamoja na Jenifer Idd, Fatuma Issa, Mariam Karama, Neema Iddy, Ashura Omary, Happiness Petar, Edna Daniel, mwajuma mussa, Ana Abdallah, Fatma Mohamed, Habiba Mohamed, na Emmy Moller,Shoo hiyo kwa mujibu wa waandaaji itaanza mchana saa nane mpaka saa moja usiku, ambapo washindi wa kwanza TV na Cheni ya Silver, wa pili na wa tatu Radio na Cheni ya Silver, wa nne na tano Cheni na washiriki wote watapata kifutia jasho kila mmoja vifaa vya shule ikiwamo madaftari, peni, na vitabu.
Waasanii mblimbli akiwamo mwanamuziki nyota Dully Sykes, Wakali Denser watakuwepo kupamba shoo hiyo, ambayo kiingilio watoto kitakuwa 1000, wakubwa 2000 na upande wa viti maalum VIP kiingilio watoto 2000 na wakubwa 4000.Onyesho hilo linadhaminiwa na Kiwanga stores & Company, A one tours & Travel, Big Respect, Alesy tours & Safari, Ngolo Trading, Afritel System Clearing & Forward, Ofisi ya Serikali za Mtaa wa 14 Temeke pamoja na Ofisi za Mazingira (Rafiki wa Mazingira),

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. UKISTAAJABU YA MUSSA UTAYAONA YA FIRAUNI!!!!!!!!!!!!!!!!!
    ACHENI ULAFI NYINYI WATU MSIO NA AIBU WALA HEKIMA.
    KAMA HAMNA KINGINE CHA KUFANYA AFADHALI MKAWA OMBAOMBA KULIKO KUTUHARIBIA WATOTO.

Post a Comment