MPOAFRIKA STUDIO YA KISASA ILIYOPANIA KUUKOMBOA MUZIKI WA BONGOFLEVA!!

Hawa ni viongozi wa Studio ya MpoAfrika iliyopo Tandika Devis Corner Wilayani Temeke studio hii imeanzishwa hivi karibuni hata hivyo tayari imeshafanya kazi nyingi za wasanii wakubwa wa muziki wa kizazi kipya bongofleva hapa nchini na wa bendi pia chini ya Producer wake Benny Mwamba, Martin Peter aliyeko kulia katika picha hii ndiyo mkurugenzi mwendeshaji, meneja wake Kerwani Amos aliyeko kushoto, hapo kati ni msanii ambaye tayari ameshafanya kazi yake katika studio hiyo Richie One, wanamuziki ambao tayari wameshafanya kazi zao katika studio hiyo ni Mr Misosi, Fid Q, Suma Lee, Insp. Haroun, Tunda Man, mwanamuziki Saleh Kupaza wa Twanga Pepeta, Chitokololo wa FM Academia na Dogo Lama na tayari nyimba zao zinagongwa katika vituo mbalimbali vya redio nchini.
Wasanii wengine ambao wanatarajia kufanya kazi yao studioni hapo ni Richie One Chiku Keto Mzimu na Juma Nature watakaporekodi wimbo wao wa pamoja unaoitwa Mukide ambao unatarajiwa kukamilika baada ya wiki mbili na kusambazwa katika vituo mbalimbali vya Redio.
Producer Benny Mwamba wa MpoAfrika Studio iliyopo maeneo ya Tandika Devis Corner akiwa Studio katika kazi zake za kila siku hapa yuko kazini akirekodi nyimbo ya msanii mwanadada Chiku Keto ambaye nimemkuta jioni hii akikamua kisawasawa studioni hapo ili kuhakikisha nyimbo yake itakapotoka mashabiki wakikubali kwa ubora wake ukitaka kufanya kzi yako katika studio hiyo unaweza kuwasiliana nao kwa namba hizi.
(0713-227979/0754-222144)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment