FM ACADEMIA KUKUAMUA RUFITA EXECUTIVE LEO!!

Wana wa FM Academia wakikamua

Watotowa mujini FM Academia wanatarajiwa kufanya shoo ya kukata na shoka kwenye ukumbi wa Rufita Executive ulioko Segerea jiji Dar es Salaam hapo Agosti 28 wakiongozwa na kiongozi wa Nyoshi El Sadaat na wanamuziki wengine kama Yelo Masai, Patchou Mwamba, Josse Mara na wengine wengi watakuletea mitindo yao kabambe kama vile Zombo na Matembele na mingine mingi.
Meneja Wa Rifita Executive Obet Msigwa amesema maandalizi yote yamekamilika kwa onyesho hilo na mashabiki wote watarajie burudani kali kutoka kwa wana Fm Academia, ameongeza kwamba kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa ni shilingi 5.000 tu na watu wote wanakaribishwa katika hilo,
Bw. Obet Msigwa ameongeza kuwa ukumbi ni Chakula na huduma nyingine zote hi kwa upande huo tuko sawasawa kabisa tuna Jiko la kisasa na wapishi wenye uzoefu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment