BONANZA LA KELKEN FITNESS, KUFANYIKA JAMAMOSI SOUTH BEACHI!!

Timu ya soka ya Fitness Veterani ya Chang’ombe kwa kushirikiana na Wanachama wa Kelken za jijini Dar es Salaam zimeandaa Bonanza la michezo katika Ufukwe wa South Beach uliopo Kigamboni ,Dar es Salaam

Akizungumzia Bonanza hilo katibu wa Kelken Fitness Rashid Nzoa alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika, na wanachama wote wamekwisha pewa taarifa na kwamba katika bonanza hilo kutashirikishwa michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba kwa watoto na watu wazima, kukimbia na magunia, kukimbiza kuku, kuogelea, pamoja na soka.
Fitness ambayo hivi karibuni ilikuwa Tanga ambako ilicheza mchezo wa kirafiki na Veterani Tanga, na kufungwa 2-1, italitumia bonanza hilo kama moja ya maandalizi ya kujiweka fiti kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Tanga kabla ya kuwavaa Veterani wa Mkoa wa Iringa .
“kazi imeanza kwa ajili ya mechi za majaribio na mikoa yote, tumeanza Tanga na tutakuwa tukicheza na mkoa mmoja mmoja ili kujipima kabla ya kushirikisha timu yetu ya vijana katika ligi ya shirikisho la soka Tanzania TFF, Tanga tulifungwa kwa taabu pamoja na kwamba katika kikosi kile kulikuwa na baadhi ya wachezaji wa Maximo lakini hata hivyo tulionyesha soka la kuvutia,”alisema Nzoa
Baadhi ya wachezaji ,Salim Salim, Christer Moyo,Nickison Terry, Mood Issa, Mary Mushi, Ally Majid, Amina Said, Salima Said, Stella Gohage, Teddy Otiego, Teddy Mushi, Joseph Asenga,Adam Nigoz, Mwastai Mgo, Bonnah Bona, John Cinna, Fatma Gulamsood, Vallentino twoo, Rya Mfaume, Fatma watoto, Fatma Gulam, na Catherine Nkeleebe
Viongozi wa timu ni, David Kiwanga (Mweka Hazina), Rashid Haruna Nzoa (Katibu), Majid A Majid (Mwenyekiti), na Ahmed Bigg ( Meneja)
Bonanza hilo pamoja na Safari zote zimedhaminiwa na Kiwanga Stores & Company, Nzowah Auto Garage, Big Respect, Karafuu Bureu de Change, Kelken Safari & Tours, Joseph Mapikipiki, Hydro Works, Technic Company Ltd, pamoja na Depo Auto Spare.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment