Na Anna Nkinda - Maelezo
Serikali imewataka askari (wa KAR) waliopigana vita kuu ya pili ya Dunia kuripoti katika ofisi za Mkuu wa mkoa au wilaya zao wakiwa na vitambulisho au vielelezo husika kwa ajili ya uthibitisho wa kutambuliwa .
Katika taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa yamehorodhesha majina ya askari wote waliopigana vita hivyo vya mwaka 1939 hadi 1945. Taarifa hiyo inasema kuwa orodha ya majina ya askari hao inapatikana katika ofisi zote za mikoa na wilaya za Tanzania bara na Visiwani.
Mikoa hiyo ni Tanga, Arusha,Mjini Magharibi , Unguja na ofisi za wilaya ya Tunduru, Songea, Nchingwea, Bunda, Serengeti, Bahi, Geita, Temeke, Kisarawe, Ilala, Maswa, Babati, Morogoro, Mvomelo, Iringa, Kyela, Singida na Dodoma mjini. Wilaya nyingine ni Kishapu, Masasi, Shinyanga, Kilosa, Karangwe, Kondoa, Tabora, Nzega, Mpanda, Kongwa, Biharamulo, Igunga, Misenyi, Muleba, Handeni, Namtumbo, mkoa wa mjini Magharibi na unguja, Wilaya ya Magharibi na Kusini Unguja.
0 comments:
Post a Comment