WASHIRIKI WA REDDS MISS KINONDONI WACHUANA VIKALI ONYESHO LA VIPAJI!!

Warembo hawa watano ndiyo walioingia katika nusu fainali ya shindano hilo la Vipaji ambapo mshindi atatangazwa katika fainali za shindano la Redds Miss Kinondoni zitakazofanyika ijumaa ya wiki ijayo tarehe 31 Agosti pale Mlimani City, shindano hili la vipaji lilifanyika janausiku kwenye hoteli ya New Africa.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akizindua rasmi shindano hilo kabala ya kuanza kwenye hoteli ya New Africa jana ambapo warembo watakaoshiriki kwenye shindano la Redds Miss Kinondoni 2009 watachuana vikali ili kumpata malkia wa kanda hiyo.




Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Mwamvita makamba pia alikuwepo kama unavyomuona akipozi katika picha mara baada ya shindano hilo kumalizika.
Mdau wetu Salome kutoka Gazeti la Citizen pia alikuwepo ili kuifahamisha jamii kilichotokea katika shindano la vipaji Redds Miss Kinondoni 2009.

Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru kulia na mama yake Miss Tanzania 2007 Richa Adhia mama yake Richa pia ni mfanyakazi wa kampuni ya Vodacom.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel kulia na Jaji mkuu wa kamati hiyo Mzee Ramesh Shah nao walikuwepo ili kushuhudia mambo yalivyokuwa yakienda.

Mwandaaji wa Redds Miss Kinondoni Boy George kati akiwa katika picha ya pamoja na Gardiner G. Habash kushoto na Dj Venture wakifuatilia kwa makini onyesho la vipaji wakati lilipokuwa likiendelea.
Mercy Garabawa kulia akiwa na wafanyakazi wake mara baada ya kuwapamba warembo.

Warembo watakaoshiriki katika shindano la Redds Miss Kinondoni wakiwa wamekaa pamoja kabla ya shindano la vipaji jana lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Huyo mercy mbona anaji-wacko namna hiyo!?

Post a Comment