Mh. Balozi wa Algeria Nchini E Abdelmoun’aam, akiwa amembeba mtoto Coletha Benedicta huku wasanii wengine wakifurahia wakati walipofanya Tafrija na kuagwa katika ubalozi wa nchi hiyo uliopo Upanga Takriban wasanii 52 na maofisa wa serikali 10 wameondoka leo kwenda nchini Algeria kushiriki katika Tamasha la Pan African Festival linaloanza Jumapili julai 5 mpaka julai 20 nchini humo FULLSHANGWE tunawatakia kila mafanikio watanzania wote wanaokwenda nchini humo kuiwakilisha nchi yetu.
Wasanii wawili ambao ni watoto lakini wana uwezo mkubwa kucheza sarakasi wa kundi la Splendid Thietre Group kutoka Ilala Coletha Benedicta kushoto na Vailet Saston ni miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania wanaotarajiwa kutisha katika tamasha la Pan Africa Festival litakalofanyika nchini Algeria kuanzia Julai 5 mpaka 20 mwaka mwaka huu wasanii hao wameondoka leo na ndege kutoka shirika la ndege la Algeria.
Kundi la ngoma za Asili la Bota kutoka kijiji cha Mtakuja Tarafa ya Lulindi Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wakipozi kwa picha nje ya Ubalozi wa Algeria tayari kwa safari yao kwenda kushiriki Tamasha la Pan African Festival litakalofanyika kuanzia julai 5 mpaka julai 20 jijini Algeris jumla ya wasanii tofauti 52 wakiongozana na maofisa wa serikali 10 wanaondoka leo kwenda nchini humo kwa ajili ya tamasha hilo.
0 comments:
Post a Comment