WAANDAAJI MISS HIGHERLEARNING WATANGAZA ZAWADI!!

Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akisisitiza jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari na waandaaji wa Miss Higherlearning leo uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Lundenga amsifu juhudi zilizofantwa na Kanda ya Vyuo vikuu katika kuboresha shindano hilo ukilinganisha na kipinfdi kilichopita kushoto ni jumbe wa Kamati ya maandalizi miss Higherlearning Zabron Mangare.
Mwanamuziki wa bendi ya African Stars Lwiza Mbutu akiimba kibwagizo cha wimbo wa Bendi hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari na waandaaji wa Miss Higherlearning kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo ambapo bendi hiyo itatoa burudani katika shindano hilo litakalofanyika ijumaa julai 3 kwenye ukumbi wa Karimjee, kulia ni mkurugenzi wa Manka Mushi Promotion Manka Mushi.

Kampuni ya Manka Mushi Promotion inayoandaa shindano la Miss Higherlearning imetangaza zawadi za washindi watakaoibuka katikashindano hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee julai 3 ijumaamwishoni mwa wiki hii, ambapo zawadi zimeboreshwa kwa kiwango cha juuhivyo itawafanya washindi wajisikie wamepata kitu kizuri, pamoja nakwamba lengo la shindano hilo ni kuwapata washiriki watakaoletaushindani katika shindano kuu la Vodacom Miss Tanzania hapo baadae.
Zawadi hizo zimepangwa katika viwango vifuatavyo ambapo malkia washindano hilo atanyakua Fanicha zenye thamani ya shilingi m. 1.500.000na fedha taslimu shilingi 500.000, Mshindi wa pili atajipatia fanichazenye thamani ya shilingi m. 1.000.000 na fedha taslimu shilingi350.000, mshindi wa tatu atapata Fanicha zenye thamani ya shilingi500.000 na fedha taslimu shilingi 250.000, Mshindi wa nne atafanyashoping katika duka la nguo la Zizzou Fashion yenye thamani yashilingi 150.000 na fedha taslimu shilingi 200.000 na wa tano atapatashilingi 100,000 na zawadi kutoka duka la nguo la City Star Boutiquewakati washiriki wengine watapata kifuta jasho cha shilingi 50.000kila mmoja.
Warembo watakaopanda jukwaani ni 12 ambao ni Mwantumu Yasuph, BeatriceKinyto, Linda Mzinga, Magreth Beatus, Dories Deonatus, Jenny Rapoo,Easther Gao, Frabcisca Mansilo, Beatrice Lukindo, Aisha Ricoh naVeronica Mick, warembo hao wako kambini katika Hoteli ya Giraffe OceanView iliyoko Mbezi Beach katika ufukwe wa bahari ya hindi wakijifuakwa ajili ya kinyang’anyiri hicho ambacho kitapewa Burudani ya kukatana shoka kutoka Bendi ya African Stars na kikundi cha burudani kutokaAsia International Youth Felloship huku kiingilio kikiwa viti maalum 20.000 na kawaida 10.000
Shindano hilo linadhaminiwa na makampuni mbalimbali kama vile Vodacom,TDL – Submiller, Ben Expedition Tours, Air Tanzania, Ndege InsuranceCo,.Tesco Furniture, Clouds FM , Leo tena, Perfect Solutions, GlobalPublishers, Billcanas, Rozella Saloon Fullshanwe.blogspo, City StarsBoutique, Dollywood, Varley Spring, Girafe Ocean View Hotel , AuroraSecurity, Carpuany Design, Hattman Production, Paka Wear, na MustafaHassanali.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment