UKAHABA : MBINU MPYA YA KUCHAPUZA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI!!

Na Ali Haji Hamad, Cape Town.
Jumuiya inyotetea haki za makahaba ya hapa Afrika Kusini imetowa wito kwa waandishi wa habari kusaidia juhudi zao za kutaka Biashara ya Ukahaba ihalalishwe na sheria za nchi kama njia ya kupunguza maambukizo mapya ya virusi vya UKIMWI.
Akizungumza na jopo la waandishi wa habari 56 kutoka zaidi ya mataifa 40 duniani, katika Kongamano lililofanyika Fountains Hotel Mjini Cape Town, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo inayojulikana kwa jina la Sex Workers Education and Advocacy Initiative, Eric Harper amedai kuhalalishwa kwa biashara hiyo kutasaidia kupunguza kiwango cha sasa cha maambukizi kwa makahaba na wateja wao kwa vile watakuwa na nguvu ya kisheria ya kuchukua hatua za kinga,
Mkurugenzi huyo ametoa wito huo zikiwa zimebakia siku mbili tu kabla ya wanasayansi, madakatari,watafiti, jumuiya zisizo za kiserikali na kiserikali, taasisi za dini na watu mmoja mmoja kuanza kukusanyika hapa kuhudhudhuria mkutano wa kimataifa wa Ukimwi unaokusudia kujadili pamoja na mambo mengine hali mbaya ya mambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, upatikanaji wa dawa za kutibu na hatua mbali mbali zilizofikiwa katika kutafuta chanjo ya ugonjwa huo.
Akizungumzia hali ya maambikizi miongoni mwa watu wanaofanya biashara ya ukahaba mkurugenzi huyo amesema katika hali ya sasa kiwango cha maambukizi miongoni mwao kinaonekana kuwa kikubwa zaidi (asilimia 9) kuliko kile cha jumla (asilimia 7) kutokana na ukweli kwamba wanoifanya kazi hiyo wanaifanya kwa magendo na katika hali ya kunyanyaswa na hawana muda wa kutosha wala nguvu za kisheria za kujadiliana njia za kujikinga kama vile matumizi ya mipira ya Condom.
Aidha ametaja sababu nyengine inayowafanya watu wanaofanya biashara ya ukahaba kuonekna na kiwango kikubwa cha maambukizi kuwa ni kuongezeka kwa kesi za kubakwa kwa wafanyabiashara hao huku wakikosa haki ya kutibiwa mapema kwa maradhi ya zinaa na haki ya kisheria ya kuwashitaki wateja wao wanaowatendea vibaya,
Mkurugenzi huyo amabaye jumuia yake inaendesha kampeni hiyo chini ya ujumbe wa MWILI WANGU BIASHARA YANGU amesema biashara hiyo ikihalalishwa matatizo yote hayo yataisha na makahaba watakuwa ni chombo muhimu cha kupambana na maambukizo mapya ya ukimwi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. MTU ULICHOKIFANYA NI KUNYUME NA ETHICS KWA TOPIC SERIOUS KAMA HIi unawezaje kuweka picha ya akina dada wa Kikorea na topic ya Afrika ya Kusini?
    Angalia utafungwa kaka

Post a Comment