Na Ali Haji Hamad, CAPETOWN
Wakati mkutano wa tano wa kimataifa wa Ukimwi ukizinduliwa rasmi leo hapa, Cape Town Afrika Kusini, Wanasayansi,wanaharakati, watafiti na viongozi wa jamii wapatao 5000 wametahadharisha juu ya uwezekano wa janga kubwa la kibinaadamu katika sekta ya afya ya kijamii iwapomataifa makubwa hayatatimiza ahadi zao walizoweka katika kupambana na janga la ukimwi duniani.
Raisi wa Jumuiya ya kimataifa ya Ukimwi IAS (Internationa AIDS Society) Julio Montana amesema kwa kusingizio cha hali ya muanguko wa kiuchumi duniani mataifa makubwa yanaonekana kusuwa sua katika kutekeleza ahadi zao kuhakikisha upatikanaji wa uhakika kwa mataifa yote duniani ya huduma za kinga na matibabu juu ya ugonjwa wa ukimwi.
" Hata kama kuna mwanguko wa kiuchumi duniani bado mwitikio wa kupambana na virusi vya ukimwi pamoja na ahadi za kutoa rasilimali za kutosha kwa kukinga na kutibu na uimarishaji mifumo ya afya kwa jumla haiwezi kupuuzwa, alisema Dr. Julio Montaner Rais wa International AIDS Society na kuongeza kuwa "Ikiwa hatutasonga mbele basi tutaporomoka kwa haraka katika vita hivi. Hu ni ukweli ambao lazima tukabiliane nao katika wakati huu ambao ugonjwa wa ukimwi unakuwa kwa kasi"
Kwa upande wake mwenyekiti mwenza wa mkutano huo kutoka katika jumuiya ya Dira Sengwe ya hapa inayoaanda kwa pamoja kati yake na IAS mkutano huo Dr. Hoosen Coovadia amesema mkutano huuu unafanyika katika wakati na pahala muafaka ambapo hapanashaka yeyote kwamba ukimwi umechangia kwa kiasi kikubwa katika kubadilisha hali ya maisha ya watu katika sekta za kisiasa ,kiuchumi na kijamii katika wakati huu wa baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi.
Mapema ufunguzi wa mkutano huo ulitanguliwa pia na maandamao yaliyoandaliwa na taasisi ya Treatment Action Campaign ya hapa na kuwajumisha watu waaoishi na virusi vya ukimwi, wahamasishaji wa mapambano na jumiya zisizo za kiserikali na wafanyakazi wa afya yalioanzia katikati ya mji na kuishia katika eneo unapofanyika mkutano huu katika ukumbi wa Cape Town International Cobvention Centre.
Katika maandamano hayo yaliyopokewa na Waziri wa afya na Ustawi wa jamii wa Afrika kusini Dr. Aaron Motsoaledi waandamanaji hao waliitaka serikali ya Raisi Jacob Zuma kuchukua hatua za kutosha kuhakikisha upatikanaji wa huduma endelevu za vidonge vya kurefusha maisha (ARVs), matibabu ya mapema kwa mama na watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi, kuongweza kwa kiwango cha watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kukubalika kutumia ARVs kutoka CD4 150 hadi 200 na kuwekwa kwa mpango wa pamoja wa kupiga vita virusi vya Ukimwi sambamba na Ugonjwa wa kifuakikuu.
Mhudumu mmoja kutoka katika Klinik ya Kailesha Cape Town alisema katika kliniki hiyo yenye wahudumu wanne pekee inalazimika kuwahudumia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi 4000 ambao wanatumia vidonge vya kurefusha maisha na akasema hali hiyo huwafanya wateja wao kusubiri muda mrefu kabla ya kupata huduma.
Waziri Aaron Motsoaledi aliahidi kwamba serikali itajitahidi kuhakikisha upatikanaji wa huduma na akatowa wito kwa watu wote waliokatika mapambano ya ukimwi kushirikiana pamoja ili kuleta mafanikio kwa watu wote wa dunia.
Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano wa kimataifa wa ukimwi unaokusanya wanasayansi, wanaharakati, watafiti na viongozi wa jumuiya zisizo za kiserikali ambao unalenga kuhaasisha upatikanani wa huduma za matibabu,utafiti na kinga kwa ugonjwa huu kufanyika Afrika.
Afrika Kusini ambapo mkutano huu unafanyika inajumla ya watu milioni tano na laki nne (4.5) wanaoishi na virusi vya ukimwi, watu laki tano (500,000) wanaoambukizwa kila mwaka ambapo 60,000 kati yao ni watoto wachanga.

0 comments:
Post a Comment