TWANGA PEPETA, MARLOW KUFANYA MAMBO MAKUBWA MISS TEMEKE 2009!!

Twanga Pepeta wakifanya vitu vyao mambo yatakuwa hivi Redds Miss Temeke 2009 TCC Sigara Chang'ombe ijumaa Agosti 1.

Msanii Marlow akiimba katika moja ya maonyesho yake.

Bendi ya African Stars "wana Dar es alaam" ama ukipenda Twanga Pepeta na Mwanamuziki Malon wanatarajiwa kutoa burudani katika shindano la Redds Miss Temeke 2009 linalotarajiwa kufanyika Agosti mosi kwenye ukumbi wa TCC sigara Chang'ombe, ambapo warembo takriban 12 wanatarajiwa kuchuana vikali katika kinyang'anyiro hicho.
Akiongea na Tovuti ya FULLSHANGWE mwandaaji wa shindano hilo kutoka kampuni ni BMP ambayo ndiyo imepewa dhamana ya kuandaa shindano hilo kwa kanda ya Temeke bw, Benny Kisaka, amesema mipango yote imekamilika hivyo kinachosubiriwa ni mashabiki watakaohudhuria katika shindano hilo kushangweka na burudani kutoka kwa wana Twanga Pepeta na Msanii maarufu na mkali katika muziki wa Bongofleva kwa sasa anayekwenda kwa jina la Malony ambaye amesumbua sana Ulaya na Marekani na kufanikiwa kujizolea mashabiki huko Ughaibuni
Ameongeza kuwa kwa sasa mazoezi yanaendelea kwenye ukumbi huohuo wa TCC Chang'ombe ambapo wapo chini ya jopo la walimu wanne ikiwa ni mwalimu wa kufundisha jinsi ya kutembea jukwaani na walimu wengine watatu kwa ajili ya kucheza shoo ya utambulisho, walimu hao ni Lona Swai Miss Temeke namba mbili mwaka jana, Bob Rich, Nyamwela kutoka Twanga pepeta na Mako Chale.
Shindano linadhaminiwa na Redds premium Cold , Vodacom, Aurora Security, Gazeti la Jambo Leo, 88.4 Clouds Fm, Mariedo Boutique, Valley Sping, Sophia Records, Raque Studio, Renzo Saloon, Mbunifu Ally Remtullah, Screen Masters tiketiza VIP zinauzwa 50.000 shilingi wasiliana na wahusika kwa namaba 0713406507.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment