Redds Miss Temeke 2009 Kusakwa Agosti 1 TCC Sigara!!

Mkurugenzi wa BMP Promotion Benny Kisaka akiongea mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo juu ya maandalizi ya shindano la kumtafuta mlimbwende atakayewakilisha kanda ya Temeke katika shindano la Vodacom Miss Tanzania litakalofanyika baadae mwaka huu.
Vimwana watakaowania taji la Redds Miss Temeke 2009 wakiwa katika pozi mara baada ya mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo.


Kwanza kabisa ningewashukuru kwa kufika kwenu leo, na kuwa wadau wakubwa si tu katika mashindano ya urembo maeneo mengine lakini hasa mlivyokuwa karibu zaidi nasi waandaji wa Redd's Miss Temeke 2009.
Kubwa leo ni kuwatangazia warembo 12 watakaopanda jukwaani Jumamosi Agosti 1, 2009 katika ukumbi wa TCC Club kuwania taji hilo linaloshikilia na Angela Lubala ambaye kwa sasa yupo masomoni nchini Marekani. Warembo hao ni Stella Solomon, Sia Ndaskoy, Shani Anthony, Irene Christopher, Celine Chipeta, Fatuma Suzan, Sara Stepehen, Christine Thomas, Samira Kafinda, Grace Shayo, Nezia Anthony na Herieth Kibambe. Hawa wanatoka katika vitongoji vya Chang'ombe, Temeke South, Kurasini na Kigamboni.
Redds Miss Temeke imedhaminiwa na Redds Premmiun Cold, Vodacom Tanzania, Aurora Security, Gazeti la Jambo Leo, Sofia Recordings, 88.4 Clouds FM(redio ya watu) nawapongeza sana kwa kuhamia katika jengo lao hii ikiwa ni moja ya hatua kubwa ya kimaendeleo nasi wanaburudani hatuna budi kuyatazama kwa mema mafanikio haya, Mwasu Fashions, 100,5 Times FM(mguso wa jamii), Screen Masters, Valley Springs, Renzo Salon, Mariedo Boutique, Fredito Entertainment, i-View Photographer na mwanamitindo Ally Rhemtullah.
Kiingilio VIP 50,000 pamoja na chakula cha jioni na sh.10,000 kawaida. Hatutakuwa na mgeni rasmi bali tutakuwa na wageni maalum wenye nyadhifa mbalimbali nchini. Burudani; Mwanamuziki Lawrance Malima 'Marlaw' mzee wa 'Jam', shoo ya safu nzima ya Twanga Pepeta na kundi mahiri la The Chocolate. *Marlow*
Redd's Miss Temeke 2009, kwanza kabisa atapata Crwon, pia ataandaliwa kila kitu na mwanamitindo Happiness Magesse ambaye kwa sasa katika kazi zake za mitindo hujutumia jina la Millen. Happiness ambaye alikuwa Miss Temeke mwaka 2001 na pia kutwaa taji la Miss Tanzania mwaka huo na kuiwakilisha nchi.
Pia mshindi huyo atazawadiwa kitita cha Sh milioni 1 na laki tano(1.5 milioni). Mwaka jana alipewa Sh. 1.2 Mshindi wetu wa pili atazawadiwa Milioni 1 wakati mshindi wa tatu atapewa kitita cha Sh laki nane(Laki 8). Hii ni zawadi iliyo juu kupita mashindano ya vitongoji kwa mshindi wa tatu. Mshindi wa nne na watano kila mmoja atajinyakulia shilingi laki tatu(laki 3) ambapo kifuta jasho kitakuwa Sh laki moja na nusu.(150,000)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment