Msanii Mtanzania wa muziki wa Hiphop anayeishi nchini Marekani Renatus Muganda aka GTK akiongea na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo asubuhi wakati alipozungumzia mkakati wake wa kukuza na kuendeleza muziki nchini ambapo ameandaa tamasha la muziki wa hiphop litakaloitwa ( Hiphop na Jamii)litakalofanyika jijini Arusha wakati wa sikukuu ya Idd Pili mwaka huu na kushirikisha baadhi ya wanamuziki wakali katika muziki huo wanaotikisa hapa nchini kama Chid Benz na wengine, Muganda amesema katika tamasha hilo anataka kuhamashisha mashule mbalimbali ili yashiriki katika tamasha hilo ambalo kiasi fulani cha pesa kitakachopatikana kitaenda kusaidia jamii
Mugada anayeishi katika jiji la Connecticut Marekani amesema amekuwa akifanya muziki wa Hiphop nchini Marekani toka mwaka 2000 na tayari ana nyimbo kama Juu kama Obama,mama,ZigZag Hussle na Thought they can be ambazo anatarajia atakamua nazo wakati wa onyesho hilo jijini Arusha.
0 comments:
Post a Comment