Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati) akipokea zawadi ya Sinia lililotengenezwa kwa mbao kutoka kwa Mwenyekiti wa maduka ya wajasiliamali wadogo ya kuuza vinyago yaliyopo karibu na maporomoko ya Victoria katika mto Zambezi Nchini Zambia Ernest Nzala huku Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Rupiah (kulia) akiangalia. Mama Kikwete ameambatana na mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Zambia
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (wa pili kulia) na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Rupiah (wa pili kushoto) wakiangalia bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na wajasiliamali wadogo wakati walipotembelea maduka hayo yaliyopo karibu na maporomoko ya Victoria katika mto Zambezi Nchini Zambia. Kulia ni waziri wa Viwanda na Biashara Nchini Tanzania Dr. Mary Nagu. Mama Kikwete ameambatana na mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Zambia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Rupi (kulia) wakiangalia maporomoko ya Victoria yaliyopo katika mto Zambezi Nchini Zambia (hayapo pichani) wakati walipotembelea maporomoko hayo jana (leo). Mama Kikwete ameambatana na mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Zambia.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Mama Kikwete atembelea soko la wajasilia wadogo na na maporomoko ya Victoria nchini Zambia!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment