WASANII WAKUBWA NDANI YA COCO BEACH, KUZINDUA ALBAMU YA MSETO WA HAPAHAPA JUMAPILI!!.

Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Video za wasanii mbalimbali wa hapa nchini waliorekodi nyimbo mbalimbali zinazopiga vita suala zima la ukimwi ambazo zimepewa jina Wahapahapa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar es alaam leo anayefuata ni Dr. Fimbo mkuu wa habari na mawasiliano katika Mpango wa Kudhibiti Ukimwi wa Taifa na Bw. Gene Peuse USAID HIV/ AIDS Control Programme

kutoka kulia ni wanamuziki Banana Zorro, Frola Mbasha na Paoul Ndunguru walipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar.

Dar Es salaam, juni 2 2009

Baada ya mafanikio y uzinduzi wa video za muziki wa mseto wa hapanahapa mwezi April, STRADCOM (strategic Radio Communication project) sasa inazindua albamu ya muziki katika TAMASHA LA BURE ufukweni coco Beach itakayo wahusisha wasanii wakubwa Tanzania kama vile Mzee YUSUPH, BANANA ZORRO, FLORA MBASHA, ENIKA, CAROLA KNASHA NA THE WAHAPAHAPA BAND, ambao wote watatumbuiza katika jukwaa moja kuanzia saa saba mchana siku yza jumapili chana june k7.
Tarehe juni 7, 2009 tamasha la Mseto wahapahapa ambayo itakuwa bure ufukweni coco Beach jijini Dar Es salaam, inaahidi kutoa burudani kwa aelfu wa watanzania kutoka kwa burudani ya hali ya juu kwa wasanii wakubwa katika sanaa ya muziki Tanzania.
Muziki na mashairi yanayoendana sambamba katika kundi hili la wasanii wakubw na maarufu Tanzania.Huku ukitoa ujumbe kadhaa kuanzia mawasiliano ya mzani-mtoto, unyanyapa, kutubu, tabia na kujali, kila nyimbo katika albamu hii imekaguliwa kwa uangalifu ili kuangaza uhalisi unaowakumba watanzania wanaoishi katika ulimwengu wa gonjwa la Ukimwi HIV.
Wahapahapa- tamthiliya ya kila wiki inayorushwa kila jumatatu kuanzia saa kumi na mbili jioni kupitia Radio Free Africa, Radio one na vituo vingine, hujishughulisha na muziki kama maigizo.Tathiliya hiyo inahusu wanamuziki chipukizi wanaojaribu kujikomboa kimaisha katika nyakati hizi za HIV/AIDS. Mradi huu umefanikishwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia United states Agency for international Development (USAID).

Maagizo haya ya wahahapa ya redio pia yanaangaza wasanii nguli juu ya maisha yao kimuziki naya kawaida.Baadhi ya wageni katika kipindi hicho ni Remy Ongola, Juma Nature, Bahati Bukuku, Ottu Jazz na wengine wengi.Baadhi ya watanzania washindi mahiri, maproduza, waigizaji na wanamuziki wamefanya kazi kwa pamoja ili kufanya wahapahapa iwe tamthililiya yenye nguvu inayoelezea misukosuko na majonzi ,matumaini na ndoto ya vijana wa sasa wakitanzania.
MSETO WAHAPAHAPA ni mchongo wa muziki kutoka kwa baadhi ya wasanii watanzania wazuri.Kupitia midundo na mashairi,wakati hawa watanzania wenye vipaji wameweza kuteka mioyo na roho ya tamthilia ya wahahapaha katika hali ambayo watanzania hawajawahi kusika au kuona.
Alprili,MFDI ilitambulisha Mseto wahapahapa video ya muziki ya DVD inazoshirikisha nyimbo za ZOBA wa Banana Zorro,CHANGANYA wa Enika,USIFE MOYO wa Flora mbasha, UJASIRI wa Carolina Kanisa,MTOTO WA MTUMAINI wa mzee yusuph, MAPAMBANO WA Bichuka na The Mlimani Park Orcherstra, SHAMBA wa Lady Jay Dee na NAISALATI wa The wa Hapahapa Band.
"Ni jambo la kufurahisha kuona jinsi gani mradi huu umeweza kukuwa na kuwa mfano wa jinsi gani sekta ya umma na sekta binafsi zinaweza kufanya kazi kwa pamoja kwa kushirikiana kusaidia maslahi ya kitaifa. Ubora wa mradi wa Mseto Wahapahapa umeweza kuwashawishi Zantel kuwekeza katika kuitangaza albamu na video ya muziki kupitia mitandao ya biashara kote nchini," Alisema John Riber- Produza Mtendaji wa Mradi wa Wahapahapa. "Mwelekezo kwa kushirikiana na Programu ya Kudhibiti Ukimwi Kitaifa (National AIDS Control Program), umewezasha video za muziki zisambazwe katika zahanati na kliniki kwa ajili ya wagonjwa kusikiliza wakisubiri wakati kutibiwa. Ni hali ya ushindi kwa wote hususan wasanii ambao wamepewa mrahaba kutokana na mauzo ya muziki/video na kutangazwa kwa matamasha kama lile tutakalokuwa nalo Juni 7 Coco Beach. Tunachukua fursa hii kuwashukuru Zantel kwa kujihusiha na tunaomba kampuni zingine kufanya kazi na sekta za umma ili kuonyesha majukumu yao katika jamii."
Tamasha hilo litarekodiwa. Usikose nafasi hii kuwa moja ya watu watakaopiga hatua ya Tanzania kufurahia sanaa ya muziki na filamu. TAMASHA LA BURE litakalohusha wasanii mahiri katika ufukwe mzuri wa Coco Beach, Jumapili mchana June 7 kuanzia saa saba mchana imedhaminiwa

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment