Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania George Francis Mangali akiongea na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo, kuzungumzia na kutolea taarifa ya mambo mbalimbali yaliyojadiliwa na bunge hilo, lililokutana nchini Burundi hivi karibuni na kujadili mambo mbalimbali kuhusu Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki,
Mh. Mangali pia amesema wadu wengi wa sekta ya Utalii katika nchi hizi wametoa maoni kuwa kusimamia utalii kwa pamoja katika jumuiya ya Afrika mashariki ni jambo zuri na litakalozifanya nchi hizi kuwa na nguvu moja katika kutangaza na kusimamia Utalii, ameongeza kuwa katika kikao hicho cha bunge la Afrika Mashariki pia Rais Piere Nkurunzinza wa Burundi alikihutubia na kupongeza Bunge hilo kwa kufanyia kikao chake hicho muhimu nchini mwake.
0 comments:
Post a Comment