WADAU WA MPIRA WASEMA KUSHINDA KWA BRAZILI MPIRA UMETENDEWA HAKI!!

Benny Kisaka ambaye ni Mnazi mkubwa wa Brazili akishangilia mara baada ya Brazili kuifunga Afrika kusini jana katika mchezo wa pili wa Nusu Fainali jana kwa matokeo hayo Afrika kusini itacheza na Italia kutafuta mshindi wa tatu na Brazili itakutana na Marekani kutafuta Bingwa wa Mabara katika mchezo utakaochezwa Jumapili nchini Afrika Kusini ambapo wadau mbalimbali walioshuhudia mchezo wa jana wamesema kushinda kwa Brazili kunamaanisha kwamba mpira umetendewa haki japokuwa Afrika Kusini nao wametisha kutokana na kiwango walichoonyesha katika mchezo huo na hii ni Dhahiri kwamba timu hiyo ya Mzee Santana itasumbua sana katika Kombe la Dunia mwaka ujao 2010 litakaloshindaniwa nchini humo.

Kutoka kulia ni Eddy kutoka Exim Bank, John Joseph Stambic Bank, Fredo na Leon wa Multchoice Tanzania nao hawakuwa nyuma kujua matokeo ya Gemu hilo tafu.
Wadau mbali mabli wakiwemo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini mpambano huo.
Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania Furaha Samalu akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mpambano wa kombe la mabara kati ya Brazili na Afrika Kusini uliokuwa ukitazamwa moja kwa moja kupitia DSTV kwenye Hoteli ya Regency Park Mikocheni.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment