Mwanamuziki wa dance Henry Galinoma anayeishinchini Uholanzi kwa kipindi cha miaka 12 sasa, makazi yake yakiwa kaskazini mwa Uholanzi katika mji wa Nieuw Buinen, anayepiga muziki wa dansi la kiafrika mashariki, jina la kisanii maarufu kama"Buti Jiwe".
Ameibuka na Albam yake mpya yenye nyimbo kumi, pini zilizomo kwenye albam hiyo ni SAMAHANI,2. MWAMY,3. SIASA.4. TUTURA TUTURA.5. KWANINI, 6. UMRI MDOGO, 7. MASHUJAA,8. MAPENZI SIO UCHAWI,9. NANI KAMA MAMA,10.MAMA YO YO huku albam hiyo ikibebwa na wimbo maarufu na unaopendwa na wengi nchini Uholanzi unaoitwa "SAMAHANI"
CD ya nyimbo zake imesambazwa katika vituo mbalimbali vya radio hapa nyumbani na baadhi ya vituo vimeanza kuzigonga nyimbo za mtanzania huyo ambaye anaibukia katika muziki wa dansi wa dance huko mamtoni na hapa nyumbani.
Siku za awali aliweza kufanya mahojiano na namtangazaji wa Radio DW, Sauti ya Ujerumani 'Bonn' Idhaa ya kiswahili Halima Nyanza aliekuwa akifanya kazi radio Uhuru ya hapa nyumbani ambako anafanya kazi hivi sasa na kwa yeyote anayehitaji CD ya mwanamuziki huyo awasiliane na muhusika kwa namba hii
0719 886 193.
1 comments:
wasanii wanahitaji juhudi sana
Post a Comment