MISS VODACOM TANGA 2009 WAZIDI KUPATA WADHAMINI!!

Baadhi ya washiriki wa shindano la Miss Vodacom Tanga 2009 linalitarajiwa kufanyika juni 16 katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

KAMPUNI ya usafirishaji Aucline Tours & Safari imeungana na wadhamini wengine waliojitosa kudhamini mashindano ya Miss Tanga 2009 ili kujitangaza zaidi kupitiamsisimko wa mashindano hayo ngazi ya mkoa.Pamoja na kampuni hiyo wadhamini wengine mbalimbali waliojikitakudhamini mashindano hayo ni Kampuni ya simu ya mkononiVodacom ambao wanasimama kama wadhamini wa kuu wa mashindanohayo na Redds Premium Cold kama wadhamini wa kuu wa mkoa huo.Wengine waliojitokeza kudhamni mashindano hayo ni Benki ya CRDBtawi la Tanga, Sofia Production, Tanga Fresh, SD Supermarket, Karata Classic,Vayle Spring, Event Lights, Excel Music, Regal Naivera Hotel, Hotel Kolaprieto,Engusero Education Center, DarWorth, Redio Breez FM, Radio Mwambao,Dollywood Tanzania, Tanga beach reasort, Aurora security, Afrique RestaurantCostal Aviation na Najim Trans.Akizungumza jana na Mwananchi, mratibu wa Miss Tanga Nassor Makau amesematayari wameingia mkataba na makampuni hayo kwa ajili ya kudhamini mashindanohayo ambayo ni kivutio kwa wadau wengi wa urembo.'Kampuni yetu, Five Brothers Entertainment inahusika na utayarishaji wamatamasha mbalimbali, tunao uzoefu wa kutosha katika shughuli hizi hapanchini na hii ni fursa adimu na muhimu kwa wadhamini kushirikiana nasi ama kufanyakazi nasi au kupata matunda ya kazi zetu, lengo letu hasa ni kuboresha mashindanohaya kuwa katika kiwango cha kimataifa, na ni wazi kuwa malengo haya ni mazitona hayawezi kukamilika bila ushirikiano wa wadhamini kama hawa,' alisema.'Tunapenda kuwashukuru sana wadhamini ambao wamejitokeza kutuunga mkono,tunajua kuwa tumefanikiwa kuwavutia wadhamini wengi kutokana na kuendeleakufanya vizuri katika maonyesho yetu yaliopita,' alisema Nassor.Fainali za mashindano ya Miss Tanga 2009 zitafanyika Juni 6 katika uwanja wa mpirawa Mkwawani ambapo zaidi ya warembo 20 watachuana kuwania taji hilo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Bongo warembo ni wazuri sana lakini wanajiharibu kwa kuchoma nywele na kujitia mkorogo, hawapendezi kabisaaaa.

Post a Comment