20 BORA WA BONGO STAR SEARCH WAANIKWA!!

Mkurugenzi wa Benchmarck Production Ritah Paulsen akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo wakati alipotangaza wasanii 20 walioingia katika 20 bora ya Bongo Star Search, ambao wako kambini na ndiyo wataanza kupigiwa kura katika shindano hilo linaloendelea tayari kwa kumpata mshindi wa mwaka huu 2009, kushoto ni Meneja Udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna
Baadhi ya Washiriki wakiwa wamepozi katika picha wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika kwenye makao makuu ya Kampuni ya Vodacom Tanzania PPF Tower.
Washiriki wa Bongo Star Search walioingia kwenye 20 bora wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati walipotambulishwa rasmi leo, washiriki hao wanatoka katika mkoa 8 kati ya mikoa 10 iliyoshirikishwa katika mchujo na kati ya hao mkoa wa Dar es alaam umetoa washiriki 8 wakati mikoa mingine 7 imetoa washiriki 12.
Waliofanikiwa kuingia 20 bora na mikoa yao ni Imani Lisu, Frola Ezekiel (Arusha) Beatrece Willliam, Pascal Cassian (Mwanza) Juma Malik, Mwampwani Yahya, Sarafina Mshindo (Dodoma) Peter Msechu (Kigoma) Leah Julius (Tabora) Issa Ahmed, Anitha Jackson, (Mbeya) Jackson George (Tanga) Alice Peter, Catherine Ntepa, Kelvin Mbati, Lulu Abdull, Maybou Mtekateka, Mary Lucas, Yacinta Richard, na Said Omary wanatoka Dar es alaam.
Washiriki watapata mafunzo zaidi ya kimuziki na kupigwa msasa ipasavyo na pia wataanza kutoa ala katika muziki wao ili waanze kupigiwa kura katika uimbaji wao Bongo Star Search inadhaminiwa na Vodacom Tanzania, Family Health International, Pepsi, Kilimanjaro Drinking Water na Presiciion Air

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment