Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 26 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. William Lukuvu, Dar es Salaam jana, kununua mabati na saruji ili kukarabati Shule ya Msingi ya Maendeleo iliyopo Temeke iliyoathirika katika milipuko ya mabomu ya Mbagala. Zain na Benki ya Stanbic wamezindua mfuko wa kusaidia maafa ya wahanga wa Mbagala unaojulikana kama ‘Saidia Maafa’.
Zain, kampuni ya simu za mkononi nchini na Benki ya Stanbic wamezindua mfuko wa kusaidia maafa ya wahanga wa milipuko ya makombora ya Mbagala, Dar es Salaam unaojulikana kama ‘Saidia Maafa’.
Akaunti ya mfuko huo iko katika Benki ya Stanbic na inaitwa ‘Maafa Account’. Watu wanaopenda kuchangia katika mfuko huo wanaweza kuweka pesa katika akaunti hiyo ya ‘Maafa Account’ kupitia akaunti namba 01400255814.
Mfuko huo wa maafa umezinduliwa Jijini Dar es Salaam leo Jumatano 5, Aprili mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. William Lukuvi na utakusanya fedha kwa ajili wa wahanga wa Mbagala. Aidha, akaunti hiyo itasimamiwa na wakaguzi maalumu wa Price Water House Coppers ambao wamejitolea kusimamia akaunti hiyo na pesa zitakazokusanywa kupitia akaunti hiyo ya Maafa Account’ zitakabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. William Lukuvi.
Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Singano Mallya alisema Zain pia imetengeneza namba maalumu, 0789 555599 ambayo watu walioguswa na janga la Mbagala wanaweza kuitumia kwa kutuma ujumbe mfupi na kuchangia katika mfuko huo.
"Wateja wetu wanaweza kutuma ujumbe mfupi wa ‘Saidia Maafa’, kwenda namba 0789 555599. Kila SMS itatozwa Tsh 250 na pesa zitakazokusanywa kupitia SMS hizo zitapelekwa kwenye akaunti ya ‘Maafa Account’ na baadaye . zitakabidhiwa kwa hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ili zisaidie katika shughuli za maafa ya Mbagala.
"Zain imeguswa sana na janga lililotokea Mbagala na kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic tunayo furaha kushiriki katika mpango huu wa kusaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia Serikali pamoja na wahanga wa janga hili. Fedha zote zitakazokusanya kutokana na ujumbe mfupi utakaotumwa na wateja wetu ambao tunaamini pia wameguswa na hili kutoka maeneo mbalimbali nchini na wangependa kuchangia katika

0 comments:
Post a Comment