Zege likishachanganywa halilali iwe usiku wa giza patawashwa taa au mchana wa jua kali na joto litabebwa tu! mpaka liishe kama unavyoona kazi hii ikiwa imepamba moto katika moja ya majengo yanayojengwa jijini mwenye ndoo haya twende, mwenye karai twende ilimradi kuchapa kazi tu, hapa ni mtaa wa makunganya posta.
Huyu nae akanaswa akivutana na mbuzi wake Posta mpya ili wakapate usafiri sasa sijui alimpandisha kwenye basi, alikodi teksi au alikodi pickup haya yote tunamwachia mwenyewe na mbuzi wake wadau.
Mwanafunzi huyu akiwa katika kituo cha mabasi cha posta asijue la kufanya kutokana na makondakta wengi kuwazuia wanafunzi kupanda katika mabasi yao wanaporejea au kwenda mashuleni na kusababisha adha kubwa ya usafiri kwa wanafunzi hapa jijini.
Huyu akipanga vizuri magazeti yake ili kujiweka sawa mara magari yatakaposimama katika foleni aweze kuyauza.
Kijana huyu akiwa kandokando ya barabara katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere TAZARA akiwa amebeba mfuko wenye chupa za Plastiki ailzookota tayari kwa kwenda kuziuza, kazi hii imekuwa ikifanywa na wakazi wengi wa jiji wanawake kwa wanaume nadhani inawapatia kipato angalau cha kukidhi shida zao.
0 comments:
Post a Comment