Waziri mkuu mstaafu Dk. John Samwel Malecela akizugumza na mkewe mama Anne Kilango Malecela ambaye ni mbunge wa jimbo la Same mashariki huku mtoto wao Dk. Mwele akiwaangalia wakati wa chakula cha mchana na watoto yatima wa kituo cha Kurasini jijini Dar es alaam, kilichokuwa kimeandaliwa maalum kwa ajili ya sherehe ya Mzee Malecela kutimiza miaka 75 jana.
Mtoto wa Mzee John S. Malecela Dk. Mwele Malecela akizungumza jambo na kuwakaribisha wageni mbalimbali waliofika katika sherehe hiyo jana Kurasini.
Kaka wa Dk. John S. Malecela Balozi Job Lusinde akipunga mkono kuwasalimia wageni mbalimbali waliofika katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kurasini katika sherehe ya kutimiza miaka 75 ya Mzee Malecela iliyofanyika jana kituoni hapo kwa kula chakula cha mchana na watoto hao.
Dada wawili wa mh. Dk John Samweli Malecela wakifuatilia kwa karibu kila kilichoendelea wakati wa chakula cha mchana ambacho mkongwe huyo wa siasa za CCM alichowaandalia watoto yatima katika kituo cha Kurasini jijini Dar es alaam wakati alipotimiza miaka 75 ya Umri wake.
0 comments:
Post a Comment