Na Anna Nkinda - Maelezo
Los Angles, Carfonia 22/04/2009
Zaidi ya wakulima 120 wa zao la pilipili aina ya paplica wamepata mafunzo ya shamba darasa ambayo yamewawezesha kulima zao hilo kwa njia ya kisasa na kuweza kupata mazao bora zaidi.
Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alipokuwa akieleza kazi za Taasisi yake wakati wa mkutano wa Afya na Uongozi kwa wake za Marais wa Afrika uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Skirball Cultural Center uliopo mjini Los Angles Carfonia.
“Ili kumwezesha mwanamke kiuchumi taasisi yangu imeanza kutoa elimu bora kwa wanawake na wanaume kuhusiana na kilimo cha kisasa darasa hili huwawezesha wanafunzi wakulima kujifunza na kuweza kulima mazao bora ambayo tayari wameshalima nasi tumewasaidia kupata masoko ya mazao yao”, alisema mama Kikwete.
Kuhusiana na vifo vya wanawake wajawazito na watoto Mama Kikwete alisema kuwa Taasisi yake inahakikisha kuwa hakuna mwanamke atakayekufa kutokana na tatizo la uzazi ndiyo maana wanatoa elimu kwa wanawake pia kuna mipango waliyojiwekea ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema, “Kuna maeneo mengine nchini Tanzania hakufikiki kirahisi hasa wakati wa mvua na wanawake wengi wanaishi vijijini pia katika zahanati nyingine hakuna vitanda vya kujifungulia WAMA tunachokifanya ni kuhakikisha kuwa vitanda vya kujifungulia vinapatikana”.
“Hadi sasa tumeshatoa vitanda kwa baadhi ya hospitali ambazo hazikuwa na vitanda vya kuzalishia ninaamini kutokana na vitanda hivyo watumishi wa afya watafanya kazi kwa bidii na kupunguza vifo vya mama na watoto wakati wa kujifungua”.
Mama Kikwete alisema kuwa kwa upande wa elimu wanamsaidia mtoto wa kike ili naye aweze kupata elimu bora ya kutosha ambayo itamsaidia kujikwamua na hali ngumu ya maisha kwani wanaamini kuwa wakimsaidia mtoto wa kike matatizo yake yataweza kutatulika kwa wakati muafaka.
“Tunaendelea kupata maombi mengi ya misaada kutoka kwa jamii yetu kwani jamii ina imani na sisi hivyo basi tunajitahidi kupanua miradi ili tuweze kuwasaidia lakini tunahitaji matreka, vifaa vya shule na mbinu za kutengeza miradi endelevu ili tuweze kufanikiwa”, alisema mama Kikwete.
Mada mbalimbali zilijadiliwa katika mkutano huo wa siku mbili ambao uliandaliwa na madaktari wa Marekani kwa Afrika ikiwa ni pamoja na jinsi ya kutokomeza vifo vya wanawake wajawazito na watoto, Ugonjwa wa UKIMWI, upatikanaji wa elimu kwa wanawake na watoto.

0 comments:
Post a Comment