KALUNDE YAPATA VIFAA VIPYA!!

Huyu ndiye mwimbaji Junior aliyejiunga rasmi na bendi ya Kalunde hivi karibuni akitokea mwanza hapa alikuwa akionyesha mambo yake makubwa katika onyesho liliofanyika mwishoni mwa wiki Hotel Peacock na hili ndilo lilikuwa onyesho lake la kwanza na Bendi hii.
Kifaa kingine kinachokwenda kwa jina la Selemani kikikung'uta Drum wakati bendi hiyo ilipofanya mambo Peacock Hotel.

Mwanamuziki mpya wa Kalunde Amos akipiga kinanda wakati wa onyesho la bendi hiyo lililofanyika Peacock Hotel mwishoni mwa wiki.

Kalunde Bandi wakiwajibika kuanzia kulia ni Deo Mwanambilimbi, Queen Vero, Hawa Kasomo na Kalunde.

Bendi ya Kalunde imefanikiwa kuwanasa wanamuziki wengine watatu katika mpango wake wa kujiimarisha zaidi ambao imeanza kuufanyia kazi katika siku za hivi karibuni ili iendane na viwango vya muziki wa kimataifa zaidi
Akizungumza na FULLSHANGWE kiongozi wa bendi hiyo kapt. Deo mwanambilimbi amesema wamefanikiwa kuwachukua wanamuziki kadhaa ambao ni Junior aliyekuwa akifanya shughuli zake za muziki mkoani Mwanza, Amos ambaye ana uwezo wa kupiga magitaa yote, kinanda pamoja na kuimba na kuna mwingine anayeitwa Kachumbari huyu anapiga Drum (Ngoma) na alikuwa anafanya shughuli zake za muziki katika nchi za Falme za kiarabu lakini pia wamempata mwingine anayeitwa Selemani huyu naye ana uwezo wa kupiga Drum (Ngoma) kuimba na kucheza.
Deo ameongeza kuwa mpango wao mwingine ni kumpata mpiga gitaa la sollo anayetokea katika ukoo wa akina Kanuti ambao karibu wote ni wanamuziki na wana uwezo mkubwa sana katika upigaji wa magitaa kwa mfano kuna Joseph Kanuti, Godfrey Kanuti na wengine wengi wanaotokea katika ukoo huo hivyo tunaamini na huyu atatusaidia kwenye bendi yetu japokuwa kwa sasa hatuwezi kumtaja mpaka mipango ya kujiunga na bendi yetu itakapokuwa imekamilika.
Deo anasema moja ya kazi nyingine ambazo wanazifanya kwa sasa ni pamoja na kurekodi Video yao mpya itakayoitwa Hilda Marugala wimbo ambao unamzungumzia mkurugenzi wa bendi hiyo ambaye haswa hili ndilo jina lake Deo anasema "lengo la kumtungia wimbo mkurugenzi wetu ni kutambua mchango wake aliouchangia mpaka bendi yetu imesimama na kuwa bendi yenye kuheshimika jijini na kwingineko katika nchi hii, hivyo tukaona hakuna zawadi ya kumpatia zaidi ya kumshukuru kwa kumtungia wimbo".
Utengenezaji wa Video hiyo inayorekodiwa ni Big Time Production unasimamiwa na Mussa Tagalile ambaye ni muongozaji mkongwe aliyetengeneza video nyingi za wanamuziki wa hapa nyumbani, Bendi ya Kalunde tayari ina video tatu toka ilipoanzishwa rasmi miaka miwili iliyopita ambazo ni Nizae na wewe, Itumbangwewe, Naomba uniambie na sasa ndiyo wanakuja na hii ya Hilda Marugala wadau kaeni mkao wa kutazama Luninga mabo mazuri yanakuja hayo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment