TANZANIA FLAVOUR UNITY YAANZISHWA!!

Menyekiti wa Tanzania Flavour Unity Lady Jay Dee kulia akiwa na katibu wake Banana Zorro


Shirikisho la wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya yaani Bongofleva linaloitwa (Tanzania Flavour Unity) limeanzishwa na tayari limekwishapata viongozi wake katika mkutano uliofanyika wiki hii siku ya jumatano katika viwanja vya Leaders Club ambapo mkutano huo uliratibiwa na mmoja wa wadau wakubwa wa muziki Ruge Mutahaba wa Radio Clouds.

Akizungumza na Tovuti ya FULLSHANGWE katibu mkuu wa shirikisho hilo ambaye amechaguliwa kwa sasa mwanamuziki na kiongozi wa bendi ya B. Band Banana Zorro, amesema mkutano wao ulifanyika vizuri na ulihudhuriwa na wanamuziki kadhaa walioitikia wito wa mkutano huo na kwa kuanzia wajumbe wa mkutano huo walichagua viongozi watakaoongoza shirikisho hilo kwa sasa.

Aliwataja viongozi waliochaguliwa na kuongoza shirikisho hilo na vyeo vyao kuwa ni Lady Jay dee ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, TID alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti, Banana Zorro alichaguliwa kuwa Katibu mkuu, Jay Moe alichaguliwa kuwa Msemaji wa shirikisho hilo, amesema katika mkutano huo waliazimia kufanya vikao kila wiki ili kuhakikisha kuwa mipango yao inakwenda kama ilivyotarajiwa.

Banana alisema lengo la kuunda shirikisho hilo ni kutekeleza baadhi ya mambo ambayo yanatakiwa kufanywa na shirikisho hilo ili kujiweka sawa kwa ajili ya kupokea msaada mkubwa ambao Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye wanamchukulia kama mfadhili wao mkubwa aliahidi kuwasaidia wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambapo aliahidi kujenga (Mastaring Studio) kubwa ya kisasa kwa ajili ya kufanyia muziki huo Mastaring hapahapa nyumbani ili uweze kuendana na soko la kimataifa.

Rais Jakaya Kikwete aliahidi kuwajengea Mastaring studio hiyo ya kisasa na ya kimataifa yenye viwango vya hali ya juu hapa nyumbani wasanii wa muziki wa kizazi kipya alipokuwa akitoa hotuba yake wakati alipoalikwa katika sherehe ya kikundi cha THT kutimiza miaka miwili hivi karibuni iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee.

FULLSHANGWE inampongeza Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa ahadi hiyo kwani wakati Mastaring studio hiyo itakapojengwa hapa nchini itachochea maendeleo ya muziki kwa wasanii wetu hapa nyumbani ili kujiweka sawa katika kuingia kwenye soko la muziki la kimataifa kama walivyo wanamuziki katika nchi nyingine zilizoendelea lakini pia itachochea maendeleo ya muziki katika ukanda huu wa Afrika Mashariki tunakupa heko Mh. Rais JK..

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment