BARCELONA KUJA TANZANIA?

Zantel kuileta Barcelona Tanzania?.
Zaingia mkataba wa miaka minne

Timu ya soka Barcelona FC ya Hispania huenda ikatembelea nchini wakati wowote kutokana na kuingia mkataba na kampuni ya simu za mkononi ya Etisalat ambayo ni kampuni mama ya Zantel inayofanya shughuli zake nchini.Etisalat imeingia mkataba wa miaka minne na Barcelona ambapo kampuni hiyo ya mawasiliano ndio itakuwa ‘Official Commmunication Patner’ katika nchi zote ambazo zinafanya kazi.Taarifa iliyotolewa na kampuni ya Zantel nchini imesema mkataba huo ambao umesainiwa juzi mjini Abu Dhabi, Oman Etisalat ina uwezo wa kuiandalia Barcelona mechi za kirafiki za kimataifa na timu ambazo zitachaguliwa na Etisalat.Mwenyekiti wa Etisalat, Mohammad Omran alisema mpira wa miguu unawakilisha kufanya kazi pamoja, uongozi, mvuto na umoja.“Etisalat imekuwa mshirika mkubwa wa mpira wa miguu na sasa imeamua kuwawashirika wa Barcelona, tunaamini kuwa soka inaweza kuwa njia sahihikuleta mabadiliko kwenye jamii, kuwaleta watu pamoja na kujenga uhusianona urafiki,” alisema.Kwa upande wake Rais wa Barcelona, Joan Laporta Estruch alisema lengo la timu yao ni kuwa na uwakilishi dunia nzima.“Lengo letu ni kuwa na uwakilishi kila sehemu, Africa, Mashariki ya Kati na Asia, hii ndio sababu klabu yetu imeamua kuingia mkataba na Etisalat moja kati ya kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano duniani, tunatarajiakufanya kazi vyema na Etisalat kwa faida ya pande zote mbili,” alisema.

Mkataba huo unaonekana utawanufaisha zaidi ya wateja milioni 80 wa Etisalat katika nchi 18 ambazo kampuni hiyo inafanya shughuli zake duniani. Wateja wa Zantel nchini wanaweza kupata taarifa mbalimbali za Barcelona kupitia simu zao na mitandao iliyo chini ya kampuni hiyo.Etisalat inadhamini ligi ya Brazilin na UAE ambapo hapa nchini inadhamini ligi ya soka Zanzibar kupitia Zanzibar ambapo pia imedhamini tamasha laSauti za Busara.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment