STARNDARD CHARTERED BANK KUKUSANYA MILIONI 21.1 KILI MARATHON, KUPAMBANA NA UPOFU!!


Benki ya Starndard Chartered imetangaza zawadi kwa washindi watakaoshiriki katika mashindani ya Kilimanjaro Marathon yanayotarajiwa kufanyika tarehe 1 mwezi machi mkoani kilimanjaro, akizungumza mkuu wa masoko ya fedha za nje Bw. Alex Bainbridge amesema jumla ya washiriki waliojiandikisha mpaka sasa ni 50 na zawadi zitakuwa katika makundi matatu ambapo kutakuwa na washiriki watakaokuwa wakishindana kwa kutumia viti maalum(Wheelchair), wengine watatumia baiskeli (Tricycle)na wengine ni walemavu wa viungo wanaoweza kushindana katika mbio hizo bila kutumia vifaa maalum.
Amesema katika makundi hayo zawadi zitatolewa kama ifuatavyo washindi wa kwanza katika makundi yote watapata kitita cha shilingi 300.000 kila mmoja, washindi wa pili watapata shilingi 150.000 washindi wa tatu watapata shilingi 125.000, washindi wa nne watapata shilingi 100.000 washindi wa tano watapata shilingi 75.000 kwa maana hiyo wanawake na wanaume wote katika mbio hizo wataondoka na zawadi ya jumla ya shilingi 4,500.000
Alex Bainbridge mesema benki hiyo imeingia katika udhamini wa Kilimanjaro Marathon ili kufanikisha katika suala la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia tatizo la upofu kwa watoto katika mradi wa "Seeng is Believing" ambao benki hiyo inashirikiana kwa pamoja na Hospitali ya CCBRT ya jijini.
Ameongeza kuwa katika mbio hizo wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi milioni 21.1 sawa na Dola 16.000 za kimarekani kwa ajili ya kazi hiyo na tayari wameshaanza kukusanya fedha hizo kwa watu mbalimbali wakiwemo wafanyakza wa Benki hiyo, katika picha kutoka kushoto anayeongea na wanahabari ni Lucy Kihwele mkuu wa Idara ya mahusiano, Alex Bainbridge mkuu wa masoko ya fedha za nje Starndard Chartered Bank, Suleiman Nyambui katibu mkuu chama cha Riadha RT na mwisho aliyesimama ni meneja uhusiano Hoyce Temu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment