RAMANI YA NJIA ZA KILI-MARATHON HADHARANI!!

Meneja Udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom Emillian Rweijuna akionyesha ramani ya njia watakazopitia wakimbiaji wa mbio za Vodacom Fun Run Km 5-8 wakati wa mbio za Kilimanjaro Marathon zinazotarajiwa kufanyika tarehe 1 mwezi machi mkoani kilimanjaro zaidi ya wanariadha 600 kutoka nchi zaidi ya 35 wanatarajiwa kushiriki katika mbio mbalimbali zitakazofanyika siku hiyo kulia katika picha ni Ibrahim Kyaruzi meneja uhusiano wa kampuni ya Executive Solution ambao ndiyo waratibu wa mbio hizo mkutano huo na wanahabari umefanyika kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo leo.

Na hii ni Ramani ya mbio za Vodacom Fun Run Km 5-8 ambazo zitakuwa ni mbio za kujiburudisha zaidi na zitakazokuwa na zawadi kemkem kutoka kampuni ya simu za mkononi Vodacom ambao ndiyo wadhamini wa mbio hizo.

Hii ndiyo ramani ya njia ambazo wanariadha watakaoshiriki katika mbio za Kilimanjaro Marathon watapitiawakati wa kukimbia mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika tarehe 1mwezi Machi zikianzia Chuo kikuu cha Ushirika na Biashara MUCCoBSna mpaka Maili Sita barabara ya Arusha kumalizikia hapohapo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment