MIKUTANO YA KIMATAIFA YA KUENDELEZA WELEDI KATIKA UTUMISHI WA UMMA KUFANYIKA TANZANIA!!.

Na Aron Msigwa - MAELEZO Dar es salaam,

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mikutano miwili ya kimataifa itakayofanyika hivi karibuni kujadili sekta ya utumishi wa umma na usimamizi wa rasilimali watu. Akitoa ufafanuzi kuhusu mikutano hiyo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Uendelezaji rasilimali watu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dr. Faiser Issa amesema kuwa mikutano hiyo inalenga kujadili maboresho katika sekta ya umma na uendelezaji wa weledi katika usimamizi wa utumishi wa umma (Professionalism).

Akizungumza kuhusu mkutano wa kwanza utakaoanza tarehe 23 hadi 27 mwezi huu Dr. Faiser amesema kuwa pamoja na mambo mengine washiriki watajadili suala la maboresho katika sekta ya utumishi na uandaaji wa rasilimali watu barani Afrika ikiwa ni pamoja na kuwa na jitihada za kuwajengea uwezo wa mameneja wasimamizi wa rasilimali watu kupambana na changamoto zinazowakabili katika utumishi wa umma barani Afrika na mikakati ya kupambana nazo.

Ameongeza kuwa licha ya mkutano huo wa kwanza kuwa na washiriki wengi Tanzania itapata faida kubwa kutokana na mkutano huo kuwa na changamoto mbalimbali za maboresho na pia kujifunza na kupata uzoefu kutoka katika nchi nyingine. “Uzoefu ambao uko kwenye nchi nyingine kuhusu utumishi wa umma utaweza kutufikia sisi watanzania na pia kwa watakaoshiriki mikutano hii, ni sehemu ya mipangilio ya kitaifa ya kuwaendeleza viongozi” amesema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mkutano wa pili utakaoanza tarehe 2 hadi 5 mwezi ujao Dr. Faiser amesema kuwa mada kuu itakuwa ni Utawala Bora na Usimamizi rasilimali Watu. Pia washiriki katika mkutano huo ambao ni watendaji wakuu katika utumishi wa umma na watumishi wanaoshughulikia taaluma ya rasilimali watu watapata fursa ya kuchambua kwa kina mfumo wa matumizi ya ajira inayofuata sifa katika maeneo yenye maamuzi mengi na kujadili faida na matatizo ya kila mfumo.

Mkutano huo wa kwanza ambao mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Dkt. Ali Mohamed Shein utagharimiwa na Idara ya umoja wa mataifa inayoshughulikia uchumi na maendeleo ya kijamii wakati mkutano wa pili ambao mgeni rasmi atakuwa waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Mizengo Pinda utafadhiriwa na Umoja wa Jumuiya ya madola wa wanataaluma wa utawala na Menejimenti (The Commonwealth Association for Public Administration).

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment