WAZIRI NGELEJA AFUNGUA WARSHA YA SERA YA MADINI 2008!!

Washiriki wa warsha ya siku mbili ya kujadili rasimu sera ya madini ya mwaka 2008 inayofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza uliopo jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Waziri wa Nisahati na madini William Ngeleja, Washiriki hao wametoka katika taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali zinazoshugulika na mambo ya madini.


Waziri wa nishati na madini Mh.William Ngeleja kushoto akijibu maswali ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu sera ya madini ya mwaka 2008 mara baada ya kufungua warsha ya siku mbili ya kujadili sera hiyo inayofanyika leo na kesho katika ukumbi wa Ubungo Plaza uliopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni katibu Mkuu wa wizara hiyo Arthur Mwakapugi picha
(Anna Nkinda wa Habari Maelezo)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment