Khalid Chuma 'Chokoraa' na Saulo John 'Ferguson' wakighani wakati Twanga Pepeta ilipotumbuiza katika onyesho la Usiku wa Zain, Dar es Salaam hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu
BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta International' kesho
(Alhamisi Desemba 4, 2008) inatarajia kuchengua mashabiki wake katika onyesho
litakalofanyika kwenye ukumbi wa Basi Haya Campsite uliopo Boko nje kidogo ya
Dar es Salaam.
Rapa na mwimbaji nguli wa bendi hiyo, Khalid Chuma 'Chokoraa', alisema Dar es
Salaam jana kuwa Twanga Pepeta inatarajia kuwachengua mashabiki wa Boko kwa
staili zake mpya za 'Sugua Kisigino' ya Saulo Ferguson na Kidude ya Chokoraa.
Chokoraa alisema Twanga Pepeta itaangusha moja moja katika onyesho
linalotarajiwa kuanza saa 3:00 usiku kwa kiingilio cha sh. 4,000 na pia
wataporomosha nyimbo mpya zinazotarajiwa kuwemo kwenye albamu ya 10 ya
bendi hiyo itakayozinduliwa mapema mwakani.
Alizitaja baadhi ya nyimbo watakazoporomosha ni pamoja na unaotamba sasa wa
Sumu ya Mapenzi ambao ni utunzi wake, Shida Darasa na Mtoto wa Mjini (Charles
Gabriel 'Chaz Baba') na Nazi Haivunji Jiwe (Thabit Abdul).

Rapa huyo alisema pia katika onyesho hilo, wanatarajia kumtambulisha mwanamuziki
mkongwe na mtunzi mahiri aliyerejea kwenye bendi hiyo, Rogart Katapila na pia
Msafiri Said 'Diouf' aliyekuwa rumande hivi karibuni, atatambulisha rap mpya za
Weka Selo na Mambo Maregea.
Wanenguaji wa bendi hiyo wanatarajiwa kuongozwa na Hassan Mussa 'Nyamwela',
Bakari Kisongo 'Mandela', Abdilahi Zungu, Lilian Tungaraza 'Internet', Maria
Soloma, Mwantumu Othman.
Pia watakuwepo waimbaji Hamis Kayumbu 'Amigolas', Saleh Kupaza, Luiza Mbutu,
Janeth Isinika, Kalala Junior na vyombo vitaporomoshwa na Abuu Semhando,
Jumanne Said 'Jojoo', Miraji Shakashia 'Shakazulu', Ismail Mzunga 'Kizunga' na
Victor Mkambi.

0 comments:
Post a Comment