Ras Nas ndani ya Dokkhuset, Trondheim, Norway

Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya muziki wa dansi na reggae, Ras Nas aka Nasibu, yuko tayari kufanya vitu vyake katika jiji la Trondheim, Norway, usiku wa Ijumaa tarehe 12 Desemba. Kwa wabongo mliopo huko msikose kuhudhuria onyesho hilo la mwaka ambapo Ras Nas ametayarisha kikosi kikali chenye wanamuziki toka Congo Brazzaville, Ivory Coast na Sweden. Kwa tahadhari, asiye na mwana itabidi aeleke jiwe! Shoo itaanza saa nne na nusu usiku. Kabla ya hapo DJ Roar Lund atakuwepo uwanjani kufyeka msitu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment