WAZIRI MKUU WA MOZAMBIQUE AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE, PATA HABARI NA PICHA!!!

Waziri mkuu wa Mozabique Dr. Luisa Dias Diogo kushoto akizungumza akizungumza na mama Maria Nyerere wakatika alipomtembelea Nyumbani kwake Msasani ili kumjulia hali Mozambique imekuwa na uhusiano wa kihistoria na Tanzania toka enzi za kupigania uhuru wa mataifa haya (Picha zote na Anna Nkinda wa Idara ya Habari Maelezo)


Mama Maria Nyerere akipata zawadi kutoka kwaMh. Waziri mkuu huyo, ni dhahiri kuwa zawadi hiyo itakuwa imemfurahisha sana mama yetu.

Dr Luisa Dias Diogo akisalimiana na mama Maria Nyerere wakati waziri mkuu huyo wa Mozambique alipomtembelea nyumbani kwake Msasani, Mozambique wanakumbuka mengi ambayo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere aliwafanyia wakati nchi hiyo ikipigania uhuru wa kujitawala kutoka mikononi wa wakoloni

Mh. waziri mkuu wa Mozambique Dr. Luisa Dias Diogo wa pili kutoka kulia na ujumbe wake waakiongozwa na mama Maria Nyerere kutembelea Bustani za mbogamboga na Matunda wakati waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini leo

Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kulia na mgeni wake Waziri mkuu wa Mozambique Dr. Luisa Dias Diogo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempiski kuzungumzia mipango mabalimbali itakayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali hizi mbili likiwemo daraja la "Umoja Unity"

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Mozambique Mh Dr Luisa Dias Diogo na mwenyeji wake waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda wakiangalia muziki wa matarumbeta wakati waziri mkuu huyo wa Mozambique alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa mwalimu Julius K. Nyerere juzi Jioni.


28/11/2008
MAGRETH KINABO – MAELEZO
DARAJA linalounganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji lijulikanalo kwa jina la ‘Umoja Unity’ linatarajiwa kukamilika Septemba mwakani ili kuwezesha mawasiliano ya kibiashara na watu baina ya nchi hizo.
Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu wa Msumbiji,Dk. Luisa Dias Diogo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ambao pia ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda uliofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam.
Dk. Diogo alisema daraja hilo linagharimu dola za Marekani milioni 30 ambazo kila nchi itachangia nusu ya fedha hizo.
“Ujenzi wa daraja hilo ni kitu muhimu kwetu,kwa kuwa litawanufaisha Watanzania na Wamsumbiji pia si kwa kwa Watanzania na Wamsumbiji hata sehemu nyingine za jirani na nchi hizi,” alisema Dk. Diogo.
Dk. alisema katika mazungumzo yake na Pinda wamekubaliana kwamba kwenye daraja hilo kijengwe kituo kimoja cha ukaguzi cha mipakani ‘One Stop Border Post’ ili kurahisisha mawasiliano ya watu na bidhaa kati ya nchi hizo.
Mawaziri hao pia wamekubaliana kwamba katika kituo hicho kuwepo na huduma nyingine kama vile uhamiaji, forodha, polisi, benki, posta mawasiliano, maji,afya na umeme.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Pinda akizungumzia kuhusu umuhimu wa daraja hilo alisema litasaidia kuimarisha mahusiahano ya kibiashara kati ya nchi hizo.
“Tunaweza tukafanya biashara za aina baina ya Tanzania na Msumbiji. Inaweza kuwa ya vyakula, samaki na bidhaa nyingine kubwa kama vile nguo ndio maana tunafikiri kuwa daraja hili ni kitu muhimu. Tunahitaji kufanya biashara halali kati ya nchi hizi mbili,” alisisitiza Pinda..
Akizungumzia kuhusu ziara yake hapa nchini, Dk, Diogo alisema kwanza anawashukuru Rais Jakaya Kikwete, pamoja na Waziri Mkuu Pinda kwa kupata nafasi ya kuzungumzia zaidi masuala ya ushirikiano kati ya nchi hizo.
Dk. Diogo alisema kwa upande wa kisiasa ushirikiano ni mzuri, lakini kwenye masuala ya kiuchumi yanahitaji kuimarishwa zaidi, ambapo aliitaja miradi ambayo inahitaji kuimarishwa kuwa likiwemo daraja hilo na miradi mingine mipya ya utalii, elimu na uhamiaji.






You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment