VIPI KANUNI ZA MISS WORD JAMANI!!



Nilisikia maneno ya Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC ambaye pia ni mlezi wa kamati ya miss Tanzania Bw. Emanuel Ole Naiko alipokuwa akitoa neno lake la shukurani na kumtakia kheri dada yetu Miss Tanzania Nasreem Ndiye, wakati alipokabidhiwa bendera ya Taifa na waziri wa mambo ya ndani Mh. Rawlence Masha, ameungana na warembo wengine Duniani katika shindano hilo kubwa la Miss Word linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Afrka ya Kusini.

Ole Naiko alisema Nanukuu "Nimemwangalia Nasreem muda mrefu tangu kule kwenye shindano la kanda ya ziwa mpaka huku kwenye shindano kubwa hapa nchini kwetu la Miss Tanzania naona kabisa anaweza kutuwakilisha vyema" mimi naungana na wewe ndugu Emanuel Ole Naiko wewe kama mlezi wa Miss Tanzania nadhani umeona kuwa kuna maandalizi ya kutosha kwa mrembo wetu kufanya vizuri katika mashindani hayo na kuiwakilisha vyema nchi yetu Tanzania.

Lakini nafikiri kuwa huenda maandalizi yetu ni ya zimamoto sidhani kama tunakuwa na maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha kuwa wawakilishi wetu katika Miss Word wanafanya vizuri ukiacha Nancy Sumari ambaye alijitutumua na kufanya vizuri hapo nyuma lakini warembo wetu wengine wengi wamekuwa wakirudi na visingizio vingi juu ya uendeshwaji wa shindano hilo la Miss Word.

kama kuna tatizo la taratibu za mashindano hayo ambazo inadaiwa zinabadilika kila mwaka je? kamati ya Miss Tanzania imeliona hilo na imejaribu kulifanyia kazi kwani ni warembo wengi ambao walienda kwenye mashindano hayo na waliporudi wakasema aidha hawakujua utaratibu uliotumika kuwapata washindi au hawakujua hata kilichojiri katika mashindano hayo katika upande wa kanuni zinazotumika kuwapata washindi.

Nadhani hili ni Suala ambalo kamati ya Miss Tanzania pamoja na kuwa inaonekana haina uwezo wa kuhoji kitu kwenye kamati ya Miss Word inatakiwa kulifuatilia kwa karibu na kujua kanuni za mashindano za kila mwaka hata kama zitakuwa zimebadilika ili kumpa taarifa mshiriki wetu ajue kuwa ni kitu gani kitaendelea ndani ya kambi mwaka huu.

Lakini pia kwa maneno haya Mzee wetu Ole Naiko na mamlaka aliyonayo kwenye kamati ya miss Tanzani ni wazi kuwa huenda maandalizi yalikuwa mazuri na yanayotarajia kutoa matunda mema katika kinyang'anyiro cha mwaka huu.

Fullshangwe inakutakia kila mafanikio Nasreem katika shindano hilo ili ukaiwakilishe nchi yetu kwa mafanikio makubwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment