TAIFA STARS YAISAMBARATISHA SUDAN 3-1 U/TAIFA!!

Timu ya Taifa ya Tanzania ikiongozwa na kocha wake mbrazil Marcio Maximo leo imetoa kipigo kikali kwa timu ya Sudan katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani yaani (CHAN), ikicheza kwa kujiamini zaidi katika uwanja mkuu wa taifa ndiyo ilikuwa ya kwanza kuandika goli lililopachika mabao matatu kupitia kwa wachezaji wake Jerry Tegete. Athman Iddi na Kigi Makassy hivyo kutokana na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Sudan tunasema hongereni sana TAIFA STARS kwa kutupa raha Watanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment