PANADOL YA MALOU STONCH YAJA!!


Mwanamuziki maarufu na wa siku nyingi Malou Stonch ambaye aliwahi kutamba na Bendi ya Stono Musica kwa sasa amerejea kwa nguvu mpya katika bendi ya FM ACADEMIA na amesema tayari katika Albam mpya ya bendi hiyo atakuwa na wimbo utakaojulikana kwa jina la (Panadol).
Malou Stonch ameyasema hayo wakati alipoongea na tovuti ya FULLSHANGWE katika mtaa wa Samora jijini leo, Malou amesema kwamba maana ya Panadol katika wimbo huo ni mapenzi yaani wanaume wanahangaika sana katika kutafuta maisha siku zote wanakumbana na vikwazo vingi .

Lakini wanawake au wake zao wanaweza kuwatuliza na kuwaliwaza waume zao na kupooza maumizvu yote wanayoyapata kutokana na kazi ngumu za kila siku hivyo nawaomba wanawake wasiwaongezee maumivu waume zao bali wawatulize na kuwapooza maumivu kwa mapenzi mema na maisha katika familia zao yataenda kwa mteremko kabisa.

Akizungumzia mapokezi aliyopewa na wanamuziki wenzake katika bendi hiyo amesema ni mazuri na yanamfurahisha, na anatoa shukurani kwa viongozi wa bendi hiyo kwani wamempokea vizuri sana na wanampa ushirikiano mzuri kitu ambacho kinayafanya mazingira ya kazi yake yawe mazuri sana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment