Lena Calist kushoto akimuonyesha Balozi Leandre Bagegwanubusa wa Burundi magari yatakayolewa kama zawadi kwa washindi wa shindano hilo ambapo magari mwawili yatashindaniwa katika Bahati nasibu magari hayo ni Lexus lenye thamani ya dola 35000, Range Rover Vogue lenye thamani ya dola 120000 na Toyota Lav4 lenye thamani ya dola 26000 uzinduzi umefanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempiski leo
Muandaaji wa Miss East Africa Lena Calist akizungumza mbele ya waandishi wa habari juu ya maandalizi ya shindano hilo litakalofanyika jijini Bujumbura Burund kulia ni Balozi wa Burundi Leandre Bagengwanubusa na kushoto ni mmoja wa maafisa wa Lena Event Shabani Mkatula
Hawa ni miongoni mwa maafisa wa kamati inayoratibu shindano la Miss East Africa chini ya Lena Calist wa kampuni ya Lena Event. kutoka kulia John Tall, Adam Kapama, Silla, na Shabani Mkatula.
Warembo waliofanya kazi ya kupokea wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja
Warembo waliofanya kazi ya kupokea wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja
Balozi wa burundi nchini Mh. Leandre A. Bagengwanubusa leo alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa shindano la Miss East Africa linalotarajiwa kufanyika 19 Desemba mwaka huu jijini Bujumbura nchini Burundi.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski balozi huyo amesema kwa sasa Burundi ni nchi ya amani sana na ili kuonyesha hilo hata viongozi wa waasi kama Agusto Loasa amerejea nyumbani ili kuendeleza nchi yake
Amewakaribisha waandishi wa habari kutembelea Burundi ili kujionea hali halisi ya utulivu ilivyo kwa sasa, ameongeza kuwa ana imani warembo watakaoshiriki katika shindano hilo watapata fulsa nzuri ya kutangaza utamaduni wa nchi zao kupitia shindano hilo.
Nae mkurugenzi wa kampuni ya Lena Event inayoratibu shindano hilo Bw. Lena Calist amesema tayari nchi kadhaa zimeshapata wawakilishi wake na zingine mpaka tarehe 1 mwezi ujao zitakuwa tayari zimewasilisha majina ya washiriki wao.
Amezitaja nchi hizo kuwa ni Reunion, Djibout, Ethiopia, Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda, Comorrow, Seachelis na Somalia.
Mshindi wa kwanza katika shindano hilo ataibuka na Gari aina ya Lexus-Rx300 lenye thamani ya dollar 35.000 na mshindi wa pili atapata dollar 5.000 na zawadi zingine lukuki kwa washindi wengine watakaofuatia pia kutakuwa na kifutajasho cha dollar 300 kwa wale watakaoishia hatua za awali.
Bw. Lena Calist ameongeza kuwa pia kutakuwa na Magari mawili mengine ambayo ni Range Rover Vogue na Toyota Lav 4 ambayo watu mbalimbali watacheza Bahati nasibu ili kushindania Zawadi hizo ambapo pesa zitakazopatikana zitakuwa ni kwa ajili ya kusaidia watoto yatima wa Burundi
0 comments:
Post a Comment