BONIFACE PAWASA (BABA UBAYA) AANZA KUTAFUNA NONDOZ CBE!!

Boniface Pawasa (Baba Ubaya) kulia akiwa na mwenyeji wake na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha biashara CBE Bw. Ally Mayay ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga
Mchezaji maarufu aliyewahi kuichezea Simba Sports Club, APR ya Rwanda na ambaye kwa sasa alikuwa akiichezea timu ya Azam FC Club inayoshiriki ligi ya Vodacom Boniface Pawasa (Baba Ubaya ) amejiunga na chuo cha biashara CBE mwezi mmoja uliopita ili kutafuna Nondoz katika chuo hicho kilichopo Wilaya ya Ilala.

Akizungumza na FULLSHANGWE ilipomtembelea chuoni hapo Pawasa amesema kwa sasa umri wake umeenda anahitaji kutengeneza maisha mapya na yenye malengo ya baadae na ndiyo maana ameamua kufuata nyayo za wachezaji wenzake waliopita kwa kujiendeleza kielimu.
Pawasa amesema kwa sasa anasomea mambo ya utawala wa biashara ambapo atakuwa chuoni hapo kwa mwaka mmoja akisomea cheti katika fani ya utawala wa biashara yaani BA, ameongeza kuwa akimaliza anatarajia kuendelea na elimu yake ya Diploma mpaka atakapokamata digrii yake ya kwanza hapo ndiyo ataangalia afanye nini.
Pawasa amesema kuwa pamoja na kwamba kocha wa timu yake ya Azam Santos anamuhitaji ili arejee kundini kuipigania timu yake katika mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom hataweza kurejea tena kwa sababu pia ana maumivu ya misuli ambayo yatamchukua muda mrefu kupona hivyo ameona asipoteze muda kusubiri apone wakati anaweza kufanya kitu kingine cha maendeleo.
Amewashukuru wachezaji wenzake kwa kumpokea chuoni hapo na anasema kwa sasa anafurahia sana maisha ya chuoni kwani rafiki zake wa karibu Ally Mayay, Aron Nyanda na Wilfred Kidilu wamempokea na wanampa sapoti ya hali ya juu na kama wao wameweza kwa nini yeye ashindwe "najua nitaweza tu na nitasoma kama nilivyojiwekea malengo yangu"anamaliza Baba Ubaya.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment