MAWAZIRI WA ZAMANI WAPANDISHWA KIZIMBANI!!

Mawaziri wa zamani katika Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Bazir Mramba (kulia) aliyewahi kuwa waziri wa Fedha na Daniel Yona aliyewahi kuwa waziri wa Nishati na madini wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa tuhuma mbalimbali za ufisadi ikiwa ni pamoja na kuisababishia serikali hasara kubwa washitakiwa wamekana mashitaka yao na mahakama imesema dhamana iko wazi kwa watuhumiwa iwapo masharti ya dhamana yatatimizwa

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment