Kesho 23/10/2008 ni siku ya umoja wa mataifa kuadhimisha miaka 63 toka uanzishwe akizungumza na mtandao wa FULLSHANGWE kaimu katibu mkuu wa chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Amir Mhando amesema UN itaadhimisha kwa kufanya tamasha la michezo pale Readers Club kinondoni.
Amesema TASWA imealikwa kushiriki katika Tamasha hilo ambapo waandishi wa habari wanawake kwa wanaume wao watashindana kuvuta kamba na kukimbia kwa magunia kwa kushindana na wafanyakazi wa UN hapa nchini
Ameongeza kwamba timu ya UN ya wanaume ya mpira wa miguu wao watacheza na timu ya wizara ya mambo ya nje ambapo zitatolewa zawadi mbalimbali amabazo ni Medali Tofauti watu mbali mbali wanakaribishwa kushuhudia michezo hiyo.
0 comments:
Post a Comment