NEW ZANZIBAR MOLDEN TAARAB YAANDAA SHEREHE BAADA YA KUZOA TUZO SABA KWA MPIGO!!!

Mwimbaji Pekee wa kiume katika kundi la New Zanzibar Molden Taarab Mhamed Mgeni akiwaongoza wenzake katika kutoa burudani kwa mashabiki wao kwenye ukumbi wa Max uliopo Ilala jana 15/10/2008 waliokaaa kutoka kulia ni Mariam Khamis, Zena Mhamed, Mwanamkuza Yumba na Mwamvita Shaibu.


Mariam Khamis na Zena Mhamed



Mwimbaji wa kundi hilo Mariam Khamis akiwa ameshika noti ya sh. elfu moja huku akipunga mkono kwa raha zake wanaofuatia ni Zena Mhamed, Mwanamkuza Yumba na Mwamvita Shaibu.


Mashabiki wa kundi la muziki la New Zanzibar Molden Taarab wakiserebuka kwa shangwe katika ukumbi wa Max uliopo Ilala jijini jana 15/10/2008

Kundi la muziki wa taarab la jijini New Zanzibar Molden Taarab limefanikiwa kujizolea takriban Tuzo saba kwa mpigo katika tamasha la utoaji wa tuzo lililoandaliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) siku ya kumbukumbu ya miaka tisa ya kifo cha baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere liliofanyika kwenye ukumbi wa Atarlight jijini.

Akizungumza na Blog hii mkurugenzi mipango wa bendi hiyo Msafiri Mwingira amesema waimbaji wao sita walipata tuzo za uimbaji bora katika Taarab hapa nchini kutokana na uwezo walioonyesha katika maonyesho mbalimbali ambayo bendi hiyo imeshirikishwa kama kundi.

Amewataja waimbaji waliotunukiwa tuzo za uimbaji bora kuwa ni Mwamvita Shaibu, Jokha Kassim, Mariam Khamis, Ahmed Mgeni, Sabah Muchacho, na Zuhura Shabaan wakati Tuzo ya saba imekwenda kwa kundi zima la New Zanzibar Molden Taarab kama Bendi Bora ya mwaka.

Ameongeza kuwa katika kusherehekea ushindi wao wameandaa Sherehe kabambe zitakazoanzia tarehe 22/10/2008 katika ukumbi wa Max pale Ilala 24/10/2008 tutakuwa na sherehe kubwa pia katika ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ally na 25/10/2008 tutakuwa na onyesho maalum la kuhitimisha sherehe zetu litakalofanyika kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo

Amemaliza kwa kuwakaribisha wapenzi na mashabiki wote wa New Zanzibar Molden Taarab kujumuika nao katika kusherehekea ushindi huo kwani mashabiki wao wamechangia kwa kiasi kikubwa Bendi yao kufikia hapa ilipo sasa hivi

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment