Wachezaji wa Yanga wakiwa katika mazoezi picha kwa hisani ya http://www.sufianimafoto.blog/
Timu ya Yanga imeishaifanyia vibaya timu ya Telecom kutoka nchini Malawi katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa Yanga mpya anayeitwa Asamoah kutoka nchini Ghana ndiye amekuwa mwiba mchungu kwa Telecom kupachika magoli matatu katika kipindi cha kwanza huku mchezaji mwingine wa timu hiyo Abdi Kassim Babi akipachika goli la nne hivyo kuifanya Yanga kwenda katika mapumziko ikiwa na magoli 4-0 dhidi ya Telecom ya Malawi.
Katika kipindi cha pili cha mchezo huo timu ya Telecom kutoka Malawi iliamka na kujitutumua ambapo ilifanikiwa kupata goli katika kipindi hicho na kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa magoli 4-1 dhindi ya timu hiyo ya wamalawi.
Huu ni mwanzo mzuri kwa timu ya Yanga kwani Agosti 14 mwaka huu inakabiliwa na mchezo mgumu wakati itakapokutana na watani wake wa jadi timu ya Simba kutoka mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam ambayo kwa sasa imejichimbia mjini Zanzibar ikitafuta dawa ya kukabiliana na Yanga katika kugombea ngao ya Hisani ya shirikisho la mpira wa Miguu nchini TFF.
0 comments:
Post a Comment