Ukweli Kuhusu Haruna Moshi ‘ Boban’ : Alikosa Namba Gavle IF


Na Maggid Mjengwa,Gavle, Sweden



HII ni sehemu tu ya makala inayohusu sakata la Haruna Moshi kukatisha mkataba na klabu ya Gavle IF. Kuna mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu Haruna Moshi kukatisha ghafla mkataba wake na klabu ya Gavle IF ya hapa Sweden. Hata hivyo, wapenzi wa soka wa Tanzania hawakuweza kupata ukweli hasa juu ya sakata la Haruna Moshi ‘ Boban’.



Nikiwa katika mji wa Gavle, mahali ambapo Haruna Moshi aliishi na kucheza kandanda ya kulipwa nimeweza kukusanya taarifa zenye kuonyesha nini kilitokea.




Kwa mujibu wa taarifa hizo, Haruna Moshi alikuwa na uwezo wa kuichezea klabu hiyo. Kilichojitokeza ni kwa Haruna Moshi kuwa majeruhi kwa muda mrefu huku nafasi ya kiungo wa kati anayoichezea ikigombaniwa na wachezaji zaidi ya watatu.Katika muda wote aliokuwa na Gefvle IF, Haruna Moshi amecheza mechi tano tu za Ligi Kuu ya Sweden.




Katika mechi hizo, ni mbili tu amecheza tangu mwanzo na nyingine tatu aliingia akitokea kwenye benchi la wachezaji wa akiba.Kwa mujibu wa maelezo ya Mkuu wa Idara ya Michezo ya klabu ya Gefle IF, Per Olson yeye anaamini, kuwa Haruna ana bahati mbaya.




Kuwa hata walipokwenda kwenye kambi ya mazoezi nje ya nchi, Haruna hakuwepo kutokana na familia yake kutarajia kupata mtoto. Hivyo, alikosa mechi tatu muhimu za kujipima nguvu na ambazo zingemweka Haruna Moshi kwenye nafasi nzuri ya kushindania namba.




Na mchezaji aliyesababisha Haruna Moshi abaki kwenye benchi ni Yussif Chibsah kutoka Ghana. Chibsah anachezea nafasi ya kiungo wa kati kama alivyo Haruna Moshi. Kurejea kwake katika klabu hiyo akitokea Ghana ndiko kulikofuta kabisa matumaini ya Haruna Moshi.




Ni nani huyu Yussif Chibsah? Na je, ilikuwa ni sahihi kwa Haruna Moshi kukatisha mkataba wake? Angeweza kubaki Sweden na kucheza katika klabu nyingine? Itaendelea… Habari hii ni kwa hisani ya


http://www.kwanzajamii.com/?p=2705 kwa habari zaidi bofya hapo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment