Hawa ni vimwana kutoka kanda ya Temeke ambayo mwaka huu inaonekana kutishia kanda zingine katika shindano la Vodacom Miss Tanzania kutokana na warembo wake kuwa katika viwango vinavyostahili katika mashindano hayo ya Vodacom Miss Tanzania hapa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupita mbele ya wageni waalikwa kwenye hafla ya kuwapongeza warembo waliofanikiwa kutinga kwenye kambi ya Vodacom Miss Tanzania ambayo itaaza hini karibuni jijini Dar es salaam.
Hafla hiyo ya kuwapongeza warembo hao iliandaliwa na kampuni ya bia ya Tanzania TBL kupitia kinywaji chake cha Redds ambao ni wadhamini wakuu wa kanda tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, hafla hiyo imefanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam ikikutanisha wadau mbalimbali wa urembo nchini.
Afisa uhusiano wa Kamati ya Miss Tanzania Aidan Rico amesema kwa njia ya simu kwamba kamati hiyo inatarajia kutangaza mbele ya wanahabari kuhusu kuanza kwam kambi hiyo siku ya jumanne ambapo kila kitu kitawekwa waazi kuhusu maandalizi ya Vodacom Miss Tanzania mwaka huu.
Hawa ni Vimwana kutoka Miss Kinondoni wakipozi kwa picha mara baada ya kupita mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo iliyoandaliwa ka wadhamini wa kuu wa kanda hizo Redds Premium Cold.
Mdau Edwin Temba wa pili kutoka kushoto na maiwaifu wake wa mwisho kushoto wakijadili jambo kuhusu zawadi katika hafla hiyo, ambapo mrembo mwenye nidhamu kutoka Miss Ilala alipewa zawadi ya Luninga nchi 18 zawadi iliyotolewa na wakuu wa kamati ya Miss Ilala.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa CM.CM. LTD Charles Mtawali, Mkurugenzi wa Fabac Fashion Aisa Idarous na Muddy Mass wakijadiliana jambo katika hafla hiyo.
Kutoka kulia ni Charels Mtawali Mkurugenzi wa Kampuni ya kuuza magari ya CM CM. LTD "Rais wa Magari" akipozi kwa picha na mfanayabiashara Muddy Mass pamoja na Gabriel Baluawa Team Freght Limited.
Kutoka kulia ni Charels Mtawali Mkurugenzi wa Kampuni ya kuuza magari ya CM CM. LTD "Rais wa Magari" akipozi kwa picha na mfanayabiashara Muddy Mass pamoja na Gabriel Baluawa Team Freght Limited.
0 comments:
Post a Comment