Wagombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, kushoto Rais Jakaya Kikwete na Mgombea Mwenza Mohamed Ghalib Bilal wakionyesha fomu zao kwa wanachama wa CCM waliowasindikiza wakati walipochukua fomu za kugombea urais kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa leo asubuhi, wagombea hao wanatarajia kurudisha fomu hizo kwenye tume ya uchaguzi Agosti 19 mwaka huu mara baada ya kukamilisha taratibu za kuzijaza, anayepiga makofi ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Pius Msekwa.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea fomu za kugombea urais kutoka kwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame leo katika ofisi za Tume hiyo jijini Dar es salaam, Wagombea hao wanatakiwa kurejesha fomu hizo Agosti 19 mwaka huu katika ofisi za tume ya Uchaguzi.
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete (kulia)na Mgombea Mwenza Mh. Mohamed Ghalib Bilal wakisaini fomu zao mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Lewis Makame hayupo pichani katika ofisi za Tume ya Uchaguzi leo hii.
Akina mama na watoto wakishangilia huku wakiwa wameshika bendera za Chama Cha Mapinduzi wakati wana CCM mbalimbali walipomsindikiza Mgombea wa urai kupitia chama hicho Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Mwenza wake Mh. Mohamed Ghalib Bilal walipochukua fomu zao katika ofisi za Tume ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment