Mwanamuziki kutoka Ivory Coast Jeff Dogolobango anayetamba na wimbo wake mpya wa (Alandji)kushoto pamoja na Meneja Mkuu Uhusiano na Mawasiliano wa Serengeti Breweriers Ltd Teddy Mapunda wakishiriki kwenye kampeni ya kufanya usafi katika Hospitali ya Mwananyamala na Kituo cha polisi cha Oysterbay leo ikiwa ni pamoja na kupiga vita ugonjwa wa Maralia kupitia kampeni ya Zinduka.
Kampeni hiyo imeshirikisha wasanii wanaoshiriki kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 "Rrrrrah", wafanyakazi wa Serengeti Breweriers pamoja na wafanyakazi wa Clouds Fm, ambapo wote kwa pamoja, wasanii walioshiriki katika zoezi hilo wanatarajiwa kupanda katika jukwaa la Fiseta Kesho kwenye Viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam
Pia wanashiriki wanamuziki wakubwa kama vile Lil Kim kutoka nchini Marekani na J. Martin kutoka Nigeria watakaowasili wakati wowote kuanzia sasa ili kuja kuwarusha mashabiki wa tamashi hilo hapo kesho.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Oysterbay Kamanda G.C.Mapunda akipaka rangi katika kuta za jengo la kituo hicho wakati wa kampeni ya kufanya usafi kituoni hapo iliyofanywa na wasanii mablimbali wanaoshiriki katika tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.
Teddy Mapunda na Mwanamuziki Keisha wakifanya usafi kwa kupiga deki katika lango kuu la kuingilia kwenye kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam leo.
Mmoja wa wakurugenzi wa Redio Clouds Ruge Mutahaba akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamanda E.J. Kalinga kushoto wakati wasanii mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Serengeti Breweriers na Clouds FM walipoenda kituoni hapo kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kupaka rangi kwenye majengo ya kituo hicho, wa pili kutoka kulia ni Meneja Mkuu Uhusiano na Mawasiliano SBL Teddy Mapunda na katikati ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Oysterbay kamanda G.C.Mapunda.
Wafanyakazi wa Serengeti Breweriers wakifanya usafi katika wodi hospitalini hapo.
Meneja Mkuu wa Uhusiano na Mwasiliano SBL Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari wakati wa kampeni ya kufanya usafi kwenye hospitali ya Mwananyamalea leo katikati ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr. Zuhura Majapa na kushoto ni Ruge Muhataba wa Clouds Fm Redio.
Kweli sio kwamba unaweza kufanya kila kitu Mtangazaji wa Redio Clouds kipindi cha Powerbreakfast Gerald Hando kushoto alishindwa kuunganisha kofia aliyopewa kwa ajili ya kutumia kwa tahadhari wakati akifanya usafi katikati ni B 12 mtangazi Clouds na kuliani Jo Makini Mwamba wa Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment