Kampuni ya Gold Star yachezesha droo!!


Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam.


Kampuni ya Gold Star leo imetangaza washindi 35 walioshindana katika bahati nasibu ya jipatie mapesa na Gold Star iliyoanza miezi miwili iliyopita wakati wa kipindi cha mashindano ya soka ya kombe la dunia.


Akiongea na wanahabari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Kulathu Srinivasan amesema lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha wananchi wapende michezo kwa ujumla..


Katika shindano hilo ambapo washindi walitambulika kwa namba, washindi 5 wa kwanza walipata kitita cha shilingi milioni 1 kila mmoja na washindi 10 walipata kitita cha shilingi laki 5 ambapo washindi 20 waliobakia walipata shilingi laki mbili na nusu kila mmoja. Alitaja lengo lingine ni pamoja na kuhamasisha watumiaji wa bidhaa za kampuni ya Gold Star kupenda michezo kwa kuangalia Kombe la dunia na kulipa moyo bara la Afrika kwa kuandaa michuano ya kombe la dunia.


“Tumefanya bahati nasibu hii ili kuwaweka pamoja wateja wetu wanaotumia rangi ya bidhaa zetu za kampuni ya Gold Star na kulipongeza Bara la Afrika kwa kupata nafasi ya kipekee ya kuandaa Kombe la dunia”.Alisema Bwana Srinivan.



Shindano hilo lilishirikisha jumla ya washiriki 35 lilianza wakati wa kipindi cha mashindano ya dunia ya mpira wa miguu na lilikuwa na lengo la kuhamasisha watanzania kuwa na utamaduni wa kupenda michezo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment