BABU WA MIAKA 108 AZUNGUMZA NA BLOG YETU,ASEMA KUJITUNZA KUNAHITAJI KULA NA KUNYWA VIZURI.

Huwezi amini huyo babu Shaban Mohamed Hanje ana umri wa miaka 108, maana yake alizaliwa mwaka 1902 lakini anatembea siku nzima akiomba misaada mbalimbali kutoka kwa watu mjini Singida.
Babu Ametoa maelezo yake juu ya umri wake na ni kwa nini ameamua kutembea mjini kuomba msaada, anasema ana watoto sita wa kike wanne na wakiume wawili lakini hawamjali hali inayosababisha atoke kijijini kwa huko Maruga Wilayani Iramba na kuja mjini ili asife njaa.
Nina miaka 108 mpaka sasa na nina nguvu za kutosha natembea kuanzia asubuhi mpaka jioni ndo narudi nyumbani kwa kijana wangu eneo la minga ambako ndiko najihifadhi.
Kama unavyomuona babu Hanje akinywa Bia aina ya kilimanjaro, kwa kweli hata wakija ndugu zangu kijijini sirudi hata kwa dawa kwani maisha ya mjini ni mazuri si unaona nakunywa bia soda na chakula mnanipa je ningekuwa kijijini ningeshakufa siku nyingi lakini nina uhakika wa kufikisha hata miaka 120, sina ugonjwa wa aina yoyote mpaka sasa niko fiti ile mbaya. Haya jamani mmesikia maeneo ya huyu Babu yetu.? kazi kwenu .
Babu akizungumza na mwanablog wetu Hillary Shoo,

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment